Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast March 26th,2022 starting 21:00 tonight

*MVUA NA NGURUMO INATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA TABORA, KIGOMA, KATAVI, KAGERA, GEITA, MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU NA MARA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UTABIRI wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo, kuanzia saa 3 usiku wa leo Machi 26,2022 unawasilishwa na mchambuzi Akili Mwangaza kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Ruvuma, Arusha, Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu na Shinyanga inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mkoa wa Iringa na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Aidha, mikoa ya Lindi, Mtwara, Kilimanjaro na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya Dodoma, Manyara, Tanga, Dar es Salaam, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia): inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Mashariki kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo huku matarajio kwa siku ya Jumatatu tarehe 28 Machi, 2022 huenda kukawa na mabadiliko kidogo.

TANZANIA WEATHER FORECAST 26/03/2022:THUNDERSHOWERS IS EXPECTED OVER SOME AREAS OF TABORA, KIGOMA, KATAVI, KAGERA, GEITA, MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU AND MARA REGIONS
 
Weather forecast for the next 24 hours starting tonight at 9:00 p.m on 26.03.2022 as presented by weather analyst Amina Saleh from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news