UVCCM Singida yaweka wazi mafanikio ya vijana kupitia uongozi wa Rais Samia kuelekea Mwaka Mmoja madarakani

NA ABDUL BANDOLA

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Singida, Dkt.Denis Nyiraha amesema, kuelekea mwaka mmoja wa uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan madarakani, miradi mingi inayotekelezwa ndani na nje ya mkoa huo imekuwa na neema kubwa kwa vijana.
"Kwa Sensa ya Mwaka 2012, Vijana wa Singida ni 822,382 sawa na asilimia 60 ya wakazi takribani 1,370,637.Hivyo wanufaika wa kwanza wa miradi yote ya maendeleo ni vijana.

"Tunaipongeza sana Serikali ya Awamu ya Sita, vile vile Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameongeza Mikopo ya Elimu ya Juu toka shilingi Bilioni 464 hadi Bilioni 570 sawa na ongezeko la shilingi Bilioni 106 ikiwa ni ongezeko la wanufaika 18,000. Leo migomo ya vyuo na Vyuo Vikuu ni historia Tanzania. Hakuna mgomo wala malumbano, Serikali inatekeleza kwa wakati,"amesema.

Dkt.Nyiraha ameyasema hayo Machi 2,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Chama Cha  Mapinduzi (CCM) kuelezea mafanikio ya Rais Samia kuelekea Mwaka Mmoja wa Uongozi wake madarakani.

Pia amesema, ndani ya mwaka mmoja wa Rais Samia katika uongozi wake jumla ya Vikundi 221 vya vijana vimenufaika na mikopo ya asilimia nne ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri hivyo kufikia lengo kwa asilimia 90 mkoani Singida.

Aidha, amesema kuwa nchi yetu imebarikiwa kwa kuwa na Rais ambaye ni Mama Mlezi na mchapa kazi.

"Kwa hiyo, tutegemee mwendelezo wa malezi bora, na tutarajie mambo makubwa mazuri kwa ajili ya ustawi bora wa uchumi
na Taifa letu,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news