Waziri Shahibu Hassan Kaduara atoa rai kwa watumishi Zanzibar

NA DOREEN ALOYCE

WAZIRI wa Maji,Nishati na Madini Zanzibar, Mheshimiwa Shahibu Hassan Kaduara amewataka watumishi wa wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na juhudi kubwa pamoja na kusimamia nidhamu za watendaji wenzao jambo ambalo litasaidia kupiga hatua zaidi.
Kauli hiyo ameitoa jijini Zanzibar wakati alipokuwa kwenye tukio la makabidhiano ya ofsi baina yake na Waziri aliyekuwepo kwenye Wizara hiyo baada ya kupangiwa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi. 

Aidha, Waziri huyo Kaduara amesema kuwa hakuna jambo jema kama ushirikiano na kama watazungumza lugha moja,nia moja, kazi itakuwa rahisi na badala ya kutawanyikana lengo la Serikali halitafikia.

"Leo nimekabidhiwa ofisi mpya ninachowaahidi ni ushirikiano uliotukuka kikubwa tuendeleze pale tulipoachiwa na Waziri ambaye amemaliza muda wake na amefanya kazi nzuri ili wananchi wetu waone faida.
"Pia niwaombe mkasimamie nidhamu ya wataalamu wenzetu tusiende kufukuza mtu,wala hakuna atakayefukuzwa na hakuna tutakayemuacha bali turekebishe tabia zetu ili kujenga ufanisi uliotukuka, tukifanya hivyo tutakuwa wamoja na kufurahia keki hii ambayo tumepewa,"amesema Kaduara.

Nae Waziri aliyekuwepo awali ambaye amehamishiwa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Suleiman Masoud Makame amewaomba watumishi kufanya kazi kwa umoja na kwamba yupo tayari kutoa ushirikiano,ushauri na maoni pale atakapotakiwa.
"Mimi nipo tayari kufanya kazi nae lile nililoanza nalo na nilipofikia ili tuweze kufikia azima ya Serikali , na nimemkabidhi mambo mbalimbali kuhusu wizara na mashirika yake ikiwemo miradi inayoendelea mikubwa,"amesema Waziri Suleiman Masoud Makame.Naibu Waziri wa wizara hiyo, Shabani Ally Othuman amesema kuwa yale yote yaliyotolewa na Waziri yatatekelezwa kiufanisi ili kazi iweze kusonga mbele.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news