Serikali yatumia Bilioni 91.1/- kulipa madeni ya mishahara ya watumishi

Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama amesema katika kipindi cha mwaka mmoja, Serikali imesimamia mageuzi makubwa kwenye Utumishi wa Umma katika kutazama maslahi ya watumishi, ikiwemo suala la upandishaji madaraja ambapo imewapandisha madaraja Watumishi wa Umma 190,781 wenye sifa stahiki na katika zoezi hilo jumla ya shilingi bilioni 39,649,988, 204 zimetumika.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa Serikali imelipa madeni ya mishahara ya Watumishi wa Umma 65,394 yenye thamani ya shilingi bilioni 91,087,826,006.34 ambayo walikuwa wakidai kwa muda mrefu.

Sanjari na hilo, Mhe. Jenista amesema, Serikali imetumia shilingi bilioni 1,330,306,572 kwa ajili ya kuwabadilisha kada na kuwalipa mishahara Watumishi wa Umma 19,386.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news