Waziri wa Afya atoa maagizo kwa watumishi

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka watumishi wa umma katika sekta ya afya kubadili fikra za utendaji kazi na kuwa wabunifu katika kutatua changamoto ili kuongeza chachu ya kufikia malengo na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Waziri Ummy amesema hayo leo Machi 30, 2022 wakati akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya,hospitali za rufaa za mikoa pamoja na taasisi zilizo chini yake uliofanyika jijini Dodoma.

“Nitoe rai kwa watumishi wote kubadili fikra zetu katika utendaji na tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii tukilenga kufikia malengo na mafanikio tuliyojiwekea. Kila mmoja katika nafasi yake awe mbunifu katika kutatua changamoto zinazomkabili na hatimaye kutoa huduma bora,"amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa madarakani ametoa Shilingi bilioni 891.5 kwa ajili ya kuboresha miundombinu pamoja na huduma za afya hivyo amewataka watumishi watumie fursa zinazopatikana zikawe chachu za kupata mafanikio makubwa Zaidi.

Akielezea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja, Waziri Ummy ametaja kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa wajawazito wanaohudhuria kniniki kwa mahudhurio manne na Zaidi, kuimarisha na kuboresha na kuboresha huduma za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi, kuimarisha huduma katika Hospitali za rufaa za mikoa.

Kwa upande wa mahusiano na wawekezaji na sekta binafsi, Waziri Ummy amesema sekta binafsi zimesaidia kujenga viwanda vya kuzalisha dawa kupitia makubaliano ya pamoja na wawakilishi wa nchi, mashirika ya kimataifa pamoja na taasisi mbalimbali.

Aidha, mafanikio mengine yaliyopatikana ni pamoja na kuimarisha huduma za uchunguzi wa magonjwa ya milipuko ikiwemo UVIKO-19 kwa kuongeza vipimo vya haraka (Rapid Test) na nija ya vinasaba (RT-PCR). kuimarisha ubora wa takwimu za mifumo kielektroniki ya ugavi wa vifaa, vifaa tiba na vitendanishi kwa ngazi zote. Kuboreshwa kwa huduma za maabara na kupata ithibati ya kimataifa.

Kwa upande mwingine Waziri Ummy ameeleza changamoto ambazo bado zinaikabili sekta ya afya ikiwemo utoaji wa huduma bora kwa wananchi hasa wa kipato cha chini, upungufu mkubwa wa watumishi wanaohitajika katika vituo vya afya, upatikanaji wa huduma za dawa, uchakavu wa miundombinu, ufinyu wa bajeti pamoja na kuondelea kuongezeka magonjwa yasiyoambukiza.

Waziri Ummy amesema changamoto hizo zitatatuliwa endapo watumishi watakuwa na ari ya utendaji wenye matokeo, uzalendo, uadilifu na ubunifu Zaidi ili kuweza kukabiliana nazo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news