JATU PLC yampongeza Rais Samia kwa kufanikisha Royal Tour kwa kishindo

NA DIRAMAKINI

TAASISI inayojishughulisha na Uwekezaji katika Kilimo nchini (JATU PLC) imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha uzinduzi wa filamu ya 'Royal Tour' na kusisitiza kuwa itazidi kulitangaza Taifa la Tanzania duniani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam siku chache baada tangu kuzinduliwa rasmi kwa filamu hiyo katika Jiji la New York nchini Marekani, Meneja wa JATU PLC, Mohamed Simbano amesema, kwa kufanikisha hatua hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan anazidi kuonyesha kwa vitendo dhamira yake ya kuiletea maendeleo Tanzania.

"Nichukue fursa hii kumpongeza Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ukweli anazidi kufanya mambo makubwa kwa Taifa hili kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani, Mungu aendelee kumlinda na kumsimamia,"amesema Simbano.

Amesema, kuzinduliwa kwa filamu hiyo inayoonyesha vivutio mbalimbali vya utalii na kitamaduni, kutazidi kuongeza idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini kwa lengo la kuja kuvitazama hatua ambayo itasaidia kukuza pato la Taifa kutokana na fedha za kigeni.

Aidha, Simbano amewataka watanzania wote kwa umoja wao kuendelea kumuunga mkono Rais Samia ili aweze kutimiza malengo yake ya kuiletea nchi maendeleo jambo ambalo pia litawezesha kuongezeka kwa kipato cha mtu mmoja mmoja.


Jumanne ya wiki hii, Rais Samia Suluhu Hassan alishiriki katika uzinduzi wa filamu hiyo ya Royal Tour ambayo pia ameshiriki kuicheza, uzinduzi ambao ulioudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo mashuhuri.

Aidha kabla ya uzinduzi huo, Rais Samia pia alishiriki mkutano na baadhi ya watu maarufu uliofanyika kwenye klabu ya faragha ya Lotos hapa New York, na miongoni mwa waliohudhuria ni Meya mashuhuri wa jiji la New York, Eric Adams, ambaye ameeleza kuipenda Tanzania na kuahidi kuitangaza zaidi katika jiji lake la New York.

Mtu mwingine mashuhuri aliyehudhuria ukiondoa mabilionea na wamiliki wa makampuni makubwa duniani ikiwemo watangazaji wa CNN, CBS nk alikuwa ni Gayle King mtangazaji mashuhuri wa vipindi vya CBC Mornings na “King in the House”.

Aidha Simbano alisema katika kuhakikisha inakuza sekta ya kilimo na maendeleo ya wananchi na Taifa kiuchumi, Jatu Plc imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali kufanikisha mipango ya kilimo katika maeneo mbalimbali nchini, lengo likiwa kuunga mkono juhudi hizo za Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news