Serikali yatoa uhakika wa maji safi na salama Kishapu, yasisitiza utunzaji vyanzo vyake

NA KADAMA MALUNDE

SERIKALI imewahakikishia wananchi wilayani Kishapu Mkoa wa Shinyanga kuwa, itaendelea kuwapatia huduma ya maji safi na salama huku ikiwataka kutunza vyanzo vya maji na miundombinu ya maji ili miradi iwe endelevu iwezesha kumtua mama ndoo kichwani kwa kumpunguzia umbali wa kufuata huduma ya maji.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe.Jasinta Mboneko (aliyevaa miwani katikati waliokaa) ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga akipiga picha ya pamoja na Wadau wa Maji Wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu. (Picha na Malunde 1 blog).

Hayo yamesemwa Aprili 22,2022 na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Jasinta Mboneko ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu ukiongozwa na Kauli mbiu ya ‘Changia huduma ya maji kwa huduma endelevu;RUWASA Maji bombani’.
Mboneko amesema serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maji pamoja na kuleta fedha kwa ajili ya miradi ya maji ili kumtua mama ndoo kichwani.

“Kwa kutambua umuhimu wa maji serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maji,tunataka kila kata ipate huduma ya maji safi na salama ili kumtua ndoo kichwani mwanamke kwa kumsogezea karibu huduma ya maji. Wajibu wa wananchi ni kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi pamoja na kulinda vyanzo vya maji pamoja na miundombinu ya maji,”amesema Mboneko.
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Jasinta Mboneko ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu. Kushoto ni Katibu Tawala wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese,kulia ni Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima.

“Niwakumbushe pia RUWASA mnapotekeleza miradi ya maji hakikisheni mnatambulisha miradi kwa wananchi ili watoe ushirikiano katika miradi hiyo. Ni lazima wananchi wafahamu taratibu na mipango yote ya miradi ili kuhakikisha miradi inatekelezeka,”ameongeza Mboneko.
Mboneko ametumia fursa hiyo kuipongeza RUWASA kwa kazi nzuri inazofanya katika kufuatilia na kutekeleza miradi ya maji huku akiwataka kuongeza kasi ya kutekeleza miradi na kubuni miradi mipya ya maji ili kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 asilimia 85 ya wananchi wilayani humo wawe wanapata huduma ya maji safi na salama kutoka asilimia 56 iliyopo sasa.

Aidha, ameiomba RUWASA kuwaunganishia huduma ya maji wananchi katika maeneo ambayo mabomba ya maji yanapita, kwani lengo la serikali ni kuhakikisha tarafa zote zinapata huduma ya maji safi na salama.
Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Neema Mwaifuge akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu. 

Mkuu huyo wa wilaya amewakumbusha watumiaji wa huduma ya maji kulipia Ankara za maji kwa wakati na kulinda miundombinu ya maji huku akiitaka RUWASA kuzikatia huduma ya maji taasisi ambazo hazilipi bili za maji.

Naye Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu, Mhandisi Dickson Kamazima amesema lengo la Mkutano huo mkuu ni kukutana na wadau wa maji kwa ajili ya kujadili, kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo katika namna bora ya utoaji huduma ya maji kwa wananchi.
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilaya ya Kishapu. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Jasinta Mboneko ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.

Amesema, RUWASA Kishapu inayo mikakati ya muda mrefu na mfupi katika kutekeleza miradi ya maji huku akieleza changamoto kubwa waliyonayo hivi sasa ni wananchi kuharibu miundombinu ya maji kwa kukata mabomba ya maji na kusababisha huduma ya maji isipatikane kama ilivyokusudiwa.

Mhandisi Kamazima amesema RUWASA Kishapu inaendelea kushirikiana na wadau wa maji kwa kupeleka huduma ya maji huku akiwataka wananchi kutunza miundombinu ya maji kwani baadhi yao wamekuwa wakiiharibu kwa maksudi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu, Emmanuel Johnson akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Emmanuel Johnson amesema wajibu wa serikali ni kutoa huduma kwa wananchi hivyo kuitaka jamii kuwafichua watu wanaoharibu miundombinu ya maji ili huduma ya maji iendelee kuwepo kila wakati.
Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese amesema serikali itahakikisha inaendelea kuleta miradi ya maji na inakuwa salama na endelevu kwa ajili ya vizazi vya sasa na vizazi vijavyo.

Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Anderson Mandia ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ukenyenge ameshauri kuwekwa kwa Luku za malipo ya kabla ‘Pre Paid’ kwa watumiaji wa maji ambao ni wadaiwa sugu zikiwemo taasisi.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Anderson Mandia ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ukenyenge akichangia hoja kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu.

Pia ameshauri kuwepo ushirikiano wa dhati baina ya viongozi wa serikali za vijiji na Vyombo wa watoa huduma ya maji ngazi ya jamii ili kuondoa malalamiko yaliyopo kumewakuwa na ushirikiano mdogo hali inayokwamisha utoaji huduma za maji.
Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hellena Paul akichangia hoja kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu. 

Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hellena Paul ameishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka huduma ya maji kwa wananchi na kuomba wananchi wa maeneo ambapo mabomba ya maji yanapita waunganishiwe huduma ya maji.

Mmoja wa Washiriki wa mkutano huo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bubiki A kata ya Bubiki, William Singu ameipongeza RUWASA kwa kasi wanayoendelea nayo katika utekelezaji wa miradi ya maji huku akibainisha kuwa ni wajibu wa vijiji husika palipo na miradi ya maji kulinda vyanzo vya maji na miundombinu ya maji.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Bubiki A kata ya Bubiki, William Singu akichangia hoja kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu.

“Suala usimamizi wa miundombinu ya maji halihitaji ulinzi wa polisi ni jukumu letu wananchi. Huku kijijini kuna viongozi na jeshi la jadi sungusungu. Ni vyema tukatambua kuwa sisi ni sehemu ya serikali hivyo ni lazima tulinde miundombinu ya maji kwani serikali inatumia gharama kubwa kuleta miundombinu ya maji,”amesema Singu.
Mchungaji wa Kanisa la KKKT wilaya ya Kishapu, Patrick Zengo akichangia hoja kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu.

Naye Mchungaji wa Kanisa la KKKT wilaya ya Kishapu, Patrick Zengo ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutatua kero za wananchi ikiwemo kuwapatia huduma ya maji huku akishauri kuwapuuza baadhi ya watu wanaobeza mambo makubwa yanayofanywa na Serikali akisema bila shaka watu hao ni mapepo.
Mhandisi wa RUWASA Kishapu, John Lupembe akiwasilisha mada kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu.
Afisa Maendeleo ya Jamii RUWASA Kishapu, Neema Mwaifuge akiwasilisha mada kuhusu Vyombo wa watoa huduma ya maji ngazi ya jamii wanasimamia huduma za maji ambapo amesema
changamoto kubwa ni wananchi kuharibu miundombinu kwa makusudi.
Mkuu wa Maabara ya Maji Mkoa wa Shinyanga, Michael Kayanda akitoa mada kuhusu usalama wa maji kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu.
Afisa Maji Mkoa wa Shinyanga, Kagoma Julius akitoa mada kuhusu Rasilimali za maji na vyanzo vya maji mkoa wa Shinyangakwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu.
Kaimu Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Masasila Maduka akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Maji wilaya ya Kishapu ulioandaliwa na RUWASA wilaya ya Kishapu ambapo amesisitiza wananchi kutunza miundombinu ya maji.

Post a Comment

0 Comments