Majaribio ya mifumo ya umeme reli ya kisasa (SGR) kuanza, TRC yatoa tahadhari kwa wananchi

NA GODFREY NNKO

SHIRIKA la Reli Tanzania (TRC) limesema kuwa, linatarajia kuanza majaribio ya mifumo ya umeme wenye ukubwa wa Volti 25000 ambao unatarajiwa kusambazwa katika nyaya za umeme za njia ya reli ya kisasa (SGR) kipande cha kwanza cha Dar es Salaam hadi Morogoro kuanzia Aprili 27,2022.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa kwa umma na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano katika Shirika la Reli Tanzania, Jamila Mbarouk.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, "Shirika linatoa tahadhari katika kipindi cha majaribio kwa wananchi na jamii inayoishi pembezoni mwa reli kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika njia ya reli ya kisasa ikiwemo kukaa, kulala, kucheza, kutembea juu ya reli, kutopita katika maeneo ambayo si rasmi, kupanda nguzo zilizopo pembezoni mwa reli ya kisasa, kuacha kushika nyaya za kusambazia umeme ambazo zimegusa ardhi kwenye tuta la reli;

Post a Comment

0 Comments