Miaka 58 ya Muungano: Pwani yawafikia waishio mazingira magumu

NA DIRAMAKINI

MKOA wa Pwani umeadhimisha miaka 58 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar (Tanzania) kwa kutoa misaada kwa vituo vya watoto waishio kwenye mazingira magumu vya wilayani Bagamoyo.

Akikabidhi misaada kwa vituo hivyo vya Moyo Mmoja na Passion Kamelot Children Home, mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema kuwa jamii inapaswa kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Kunenge amesema kuwa, jamii ni familia kubwa hivyo kuwasaidia watu wenye uhitaji ni kuisaidia familia.

Amesema kuwa, wametoa misaada hiyo ili kuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akipambana kuhakikisha anapunguza changamoto kwa wananchi.

Aidha, amewataka wananchi kushiriki kikamilifu wakati wa zoezi la sensa ya watu na makazi ili nchi iweze kujua idadi ya watu na kupanga bajeti kutokana na idadi ya wananchi wake.

Naye Sister Asteria Pantaleo ambaye ni mlezi wa kituo cha Passion Kamelot Children Home amesema kuwa wananchi wanaokaa jirani na kituo hicho wanamahitaji mengi ya kijamii.

Kwa upande wake Apaisaria Minja Meneja wa Kituo cha Moyo Mmoja amesema kuwa, wanaomba wanafunzi wanaohitimu elimu ya Msingi wanaotoka kwenye kituo hicho kupangiwa shule za mbali ili kubadili mazingira.

Post a Comment

0 Comments