MO Green International yazindua bidhaa ya kuua wadudu wanaoshambulia zao la pamba

NA EMMANUEL MBATILO

KAMPUNI ya Mo Green International inayojihusisha na uagizaji na usambazaji wa pembejeo za kilimo nchini imezindua bidhaa yao mpya ya Mo Strong ambayo ni kiuadudu ambacho kina uwezo wa kuua wadudu wa kufyonza na kukata kwenye pamba na mazao mengine.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mo Green International, Bw. Matolo Patrick akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitambulisha bidhaa yao mpya ya Mo Strong ambayo kazi yake ni kuua wadudu wanaoshambulia zao la pamba.

Akizungumza leo Aprili 8,2022 na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mo Green International, Bw.Matolo Patrick amesema, kiuwatilifu hicho kinaua kwa kiasi kikubwa, kwani kiambata chake cha LAMDACYHALOTHRIN 101g/I+THIAMETHOXAM 141g/I ni bora ndani yake.

Amesema, kwenye zao la pamba kuna matatizo mengi hasa ya wadudu mbalimbali, kuna wadudu wanaokata au kutafuna mazao na kuna wadudu wanaofyonza pamba na kusababisha pamba kwenda kwenye daraja la pili badala ya kwenda kwenye daraja la kwanza.

"Hawa wadudu wanasababisha mkulima kupunguza mapato kutoka asilimia 70 mpaka 90, kwa hiyo kampuni yetu ipo kwa ajili ya kumlinda mkulima wa pamba sehemu hiyo,"amesema.

Aidha, amesema lengo kubwa la kampuni hiyo ni kushirikiana na wakulima kuhakikisha wakulima wanapata mafunzo sahihi kwenye utumiaji wa viuatirifu na kwenye kulinda mazao yao ili kuongeza kipato na kupata mazao yaliyo bora zaidi. Afisa Kilimo wa Kampuni ya Mo Green International, Bw.Alex Michael akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitambulisha bidhaa yao mpya ya Mo Strong ambayo kazi yake ni kuua wadudu wanaoshambulia zao la pamba.

Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Kampuni ya Mo Green International, Bw.Alex Michael amesema, dawa ya Mp Strong ina uweo mkubwa wa kuangamiza wadudu ambao wanashambulia pamba, hivyo wana vipimo ambavyo wameviweka kwa ajili ya kutumika kwa mkulima anayetumia kupambana na hao wadudu.

"Tumeweka vipimo ambapo mtu akitumia bomba lenye ujazo wa lita 16 tunashauri atumie miezi 15 mpaka miezi 20 na kwa yule ambaye atakuwa anatumia bomba la lita 20 yeye tutashauri apime miezi 19 mpaka miezi 24,"amesema Michael.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news