NMB yatoa ufadhili kwa wanafunzi 200,madawati

NA DIRAMAKINI

BENKI ya NMB itatoa ufadhili wa elimu kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita na vyuo vikuu 200 wanaotoka kwenye mazingira magumu na wenye ufaulu mzuri kwa mwaka huu.

Aidha, NMB imetoa viti 50 na meza 50 vyenye thamani ya shilingi milioni tano kwenye Shule ya Sekondari ya Mwanalugali kwa ajili ya kupunguza changamoto za shule hiyo.

Hayo yamesemwa mjini Kibaha na Mkaguzi wa ndani wa benki hiyo, Benedicto Baragomwa wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari ya Mwanalugali.
Baragomwa amesema kuwa mwaka jana NMB ilizindua asasi ya kiraia inayoitwa NMB Foundation ambapo kuna kitu kinaitwa Nuru Yangu Scholarship na Mentorship Program ambayo inatoa ufadhili wa masomo.

"Ufadhili huu ni wa masomo kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita na kwa wale wanaoingia vyuoni kigezo kikubwa uwe umefaulu vizuri na pia wanaotaka familia duni,"alisema Baragomwa.

Baragomwa amesema kuwa, ama imani kuwa wahitimu wote hawa wataendelea na masomo katika vvuo vikuu hivyo washike masomo na wasome kwa bidii sana, "kwani siku hizi vijana wamejenga dhana kuwa elimu bora inapatikana nje ya nchi, yaani majuu ambapo hiyo ni dhana potofu, elimu ya Tanzania ni bora sana na tujivunie,"alisema.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Joseph Mkumbo alisema kuwa, changamoto kubwa iliyopo ni kutokuwa na uzio hali ambayo inasababisha baadhi ya wanafunzi hasa wavulana kutokana maeneo mengi kutoendelezwa na kusababisha matokeo kuwa mabaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news