Polisi waendelea na uchunguzi kifo cha Padri Francis Kangwa

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kiuchunguzi linaendelea kuchunguza kwa kina kifo cha Padri Francis Kangwa (49) raia wa Zambia aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Mbezi Mshikamano iliyopo Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Akitoa taarifa hiyo Aprili 19,2022 jijini Dar es Salaam, Kamanda wa kanda hiyo, ACP Muliro Jumanne Muliro amesema, Padri huyo alikutwa amefariki ndani ya tenki kubwa la maji lililopo nyuma ya nyumba ya makazi ya Mapadri iliyopo Mtaa wa Sokoine katika jengo la Ottoman jijini Dar es Salaam.

Aidha, amesema Padri huyo alifika katika Kanisa la St.Joseph lililopo Mtaa wa Sokoine Aprili 12,2022 kwa ajili ya ibada maalum, na mara baada ya ibada alielekea kwenye makazi ya mapadri kujipumzisha, lakini hakuonekana mpaka Aprili 15,2022 alipokutwa amefariki eneo hilo.

“Uchunguzi wa awali kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kiuchunguzi unaonesha dalili kwamba Padri huyo anaweza kuwa amejiua, hata hivyo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini sababu halisi iliyopelekea kifo cha Padri huyo,”amesema ACP Muliro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news