Rais Samia kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya Royal Tour

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan atashiriki uzinduzi wa makala maalumu iitwayo ‘Royal Tour’ leo jijini New York nchini Marekani.
Filamu hiyo ambayo mchakato wake umefanyika karibu mwaka mzima umemshirikisha Rais Samia na umeangazia vivutio mbalimbali vya utalii na imelenga kuongeza watalii na kuvutia wawekezaji.

Washiriki wengine ni Wakuu wa taasisi za biashara za kimataifa, waongoza utalii wa kimataifa, viongozi wa kisiasa, mashirika ya kimataifa, waandishi wa habari na watanzania waishio marekani.

Wafadhili na wau mbalimbali zikiwemo taasisi za uhifadhi kama Tanapa, NCAA, TTB, TAWA, TFS na makundi ya wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania wakiwakilishwa na CTI, TBA, TPSF, TATO na CEOrt wanahudhuria.

Post a Comment

0 Comments