Simba SC yawagonga US Gendarmerie '4G' ya viwango vya Kimataifa

NA DIRAMAKINI

UBAO wa Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam umesoma Simba 4 huku US Gendarmerie ukisoma 0 baada ya dakika 90 kutamatika katika mchezo wa makundi.
Wagongaji kwa Simba SC ni Sadio Kanoute dakika ya 63,Chris Mugalu dakika ya 68 na 78 na kipa wa wageni hao alijifunga dakika 84.

Kwa matokeo hayo ya Simba SC kukomba alama zote na mabao ya kutosha,ipo nafasi ya pili na alama 10 kundi D sawa na RS Berkane.
Aidha,timu mbili zinapita zote zikiwa zimekusanya alama 10 kibindoni tofauti ikiwa ni mabao ya kufungana. 

Wekundu wa Msimbazi wanatinga hatua ya robo fainali ikiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kuongeza utulivu uliowazalia matunda.

Katika dakika za kwanza wawili hao walionekana kutoshana nguvu, hivyo kwenda mapumziko ubao ukisoma sufuri kila upande.
Simba SC walikwama kutupia kupitia kwa Pape Sakho aliyekosa nafasi mbili, Sadio Kanoute nafasi tatu za kufunga.

Pia Kanoute kwa kucheza faulo ameonyeshwa kadi ya njano na mwingine kwa Simba ni Joash Onyango ambaye hakuwa na chaguo alimchezea faulo Adebayo Victorean. Simba wamepiga kona 10 USGN 0 huku mashuti yakiwa 10 na moja limelenga lango.

Post a Comment

0 Comments