TRA yakusanya Trilioni 16.7/-, hizi hapa sababu

*Ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.3 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 17.15/-

NA GODFREY NNKO

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) katika kipindi cha robo tatu kwa maana ya mwezi Julai hadi Machi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 imekusanya shilingi trilioni 16.69 ikiwa ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.3 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 17.15.
Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa leo Aprili 3,2022 na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Alphayo J. Kidata.

Bw.Kidata amesema kuwa, makusanyo hayo ni ongezeko shilingi trilioni 3.1 ukilinganisha na kiwango cha makusanyo cha shilingi trilioni 13.59 kilichokusanywa kipindi kama hicho kwa mwaka wa fedha 2020/21.

"Ongezeko hili ni ukuaji wa asilimia 23.17. Aidha, kwa mwezi Machi 2022, TRA imekusanya shilingi trilioni 2.06 kati ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 1.98. Makusanyo haya ni sawa na ufanisi wa asilimia 103.6 na ukuaji wa asilimia 23.17 ikilinganishwa na mwezi Machi 2021 ambapo makusanyo yalikuwa shilingi trilioni 1.67.

"Ifahamike kuwa, makusanyo haya kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na kuongezeka kwa uhiari wa kulipa kodi, kuimarika kwa mahusiano baina ya TRA na walipakodi kunakochagizwa na utatuzi wa migogoro ya kodi nje ya mahakama.

"Pamoja na kushughulikia malalamiko ya walipakodi kwa wakati, kadhalika, ufanisi huo umetokana na kuimarika kwa uzalishai wa viwanda vya ndani na biashara za Kimataifa,"amefafanua Bw.Kidata.

Wakati huo huo, Bw.Kidata amesema, TRA inawapongeza walipa kodi wote na wadau mbalimbali kwa kujitolea kwa dhati katika kuendelea kulipa kodi kwa hiari.

"Kipekee, tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo na msaada wake katika kutekeleza wajibu wetu.

"Ulipaji kodi sahihi, wa hiari na kwa wakati kumeifanya TRA ivuke lengo mwezi Machi 2022 na kuiwezesha Serikali kutekeleza majukumu yake kwa wananchi kama vile kugharamia miradi ya maendeleo, kutoa huduma za kijamii, ulinzi na usalama wa nchi,"amesema.

Wito wa TRA

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news