Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 14th,2022 starting 21:00 tonight

*VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KILOMITA 40 KWA SAA VINATARAJIWA KATIKA MAENEO MACHACHE YA MWAMBAO WA PWANI YA BAHARI YA HINDI (MIKOA YA LINDI NA MTWARA IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA) PAMOJA NA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WA ZIWA NYASA (MIKOA YA RUVUMA NA NJOMBE)

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia leo saa tatu usiku Aprili 14,2022 unaletwa na mchambuzi Tunza Sanane kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, Visiwa vya Unguja na Pemba, Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Pwani (visiwa vya Mafia) inatarajiwa kuwa na mawingu, mvua na ngurumo kwa maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

Aidha, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe, Iringa, Mbeya, Njombe, Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara inatarajiwa kuwa na mvua na ngurumo na vipindi vya jua.

Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha inatarajiwa kuwa na mvua nyepesi na vipindi vya jua huku Tabora, Manyara, Dodoma na Singida ikitarajiwa kuwa na jua.

Wakati huo huo, upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kusini Mashariki kwa kasi ya kilomita 40 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.

Katika hatua nyingine, kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi hadi makubwa.

WEATHER FORECAST 14/04/2022:STRONG WIND IS EXPECTED OVER LINDI, MTWARA, NJOMBE AND RUVUMA REGIONS
Weather forecast as presented by analyst Magreth Massawe from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news