Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 20th,2022 starting 21:00 tonight

*MVUA NA NGURUMO INATARAJIWA KATIKA MAENEO YA KANDA YA ZIWA NA KASKAZINI

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku leo Aprili 20, 2022 unawasilishwa na mchambuzi Akili Mwangaza kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, visiwa vya Unguja na Pemba, mikoa ya Kigoma, Katavi, Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

Aidha, mikoa ya Tanga, Tabora, Arusha, Manyara na Kilimanjaro inatarajiwa hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) inatarajiwa hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Morogoro, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Rukwa, Songwe, Iringa, Mbeya na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Wakati huo huo kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, mikoa ya Dodoma na Singida inatarajiwa hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

TANZANIA WEATHER FORECAST 20.04.2022:THUNDERSHOWERS IS EXPECTED OVER AREAS OF LAKE VICTORIA BASIN AND NORTHERN PARTY
Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight 20/04/2022 presented by weather analyst Mohamed Hamis from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Post a Comment

0 Comments