Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 22nd,2022 starting 21:00 tonight

*MVUA INATARAJIWA KATIKA NCHI NZIMA

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku wa leo Aprili 22, 2022 unaletwa na mchambuzi Tunza Sanane kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, Kigoma, Tabora, Katavi, Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara inatarajiwa kuwa na mawingu, mvua na ngurumo kwa maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.

Aidha, Dar es Salaam, Tanga, Lindi, Mtwara, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia) na visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na mvua na ngurumo kwa maeneo machache na vipindi vya jua.

Mikoa ya Rukwa, Arusha, Manyara na Kilimanjaro inatarajiwa kuwa na mvua na jua huku Dodoma, Singida, Morogoro, Ruvuma, Songwe,Iringa, Mbeya na Njombe ikitarajiwa kuwa na mvua nyepesi na jua.

Wakati huo huo, upepo wa Pwani kwa mujibu wa TMA unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini Mashariki kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote huku hali ya bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi madogo.

TANZANIA WEATHER FORECAST 22.04.2022: RAINFALL IS EXPECTED OVER THE ENTIRE COUNTRY.
Amina Salehe from Tanzania Meteorological Authority (TMA) is today's weather analyst.

Post a Comment

0 Comments