Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast April 9th,2022 starting 21:00 tonight

*MVUA NA NGURUMO INATARAJIWA MAENEO MACHACHE YA RUVUMA, KAGERA NA GEITA

NA GODFREY NNKO

UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku wa leo Aprili 9,2022 unaletwa na mchambuzi Daniel Masunga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Kagera, Geita na Ruvuma inatarajiwa kuwa na mvua, ngurum na vipindi vya jua.

Huku Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Visiwa vya Unguja na Pemba, Njombe, Songwe na Mbeya ikitarajiwa kuwa na mvua na vipindi vya jua.

Wakati huo huo, kwa mujibu wa TMA mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Lindi na Mtwara inatarajiwa kuwa na mvua nyepesi na vipindi vya jua.

Aidha, mikoa ya Mara, Simiyu, Shinyanga, Mwanza, Kigoma, Katavi, Tabora, Manyara, Singida, Dodoma na Rukwa inatarajiwa kuwa na jua.

Katika hatua nyingine, upepo wa Pwani kwa mujibu wa TMA unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kusini kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kusini ambapo hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi.

WEATHER FORECAST 09/04/2022;THUNDERSHOWERS IS EXPECTED OVER FEW AREAS OF RUVUMA, KAGERA AND GEITA
Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight 09/04/2022, presented by analyst Daniel Masunga from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news