Rais Samia:Tuendeleze Falsafa za Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema, Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa kiongozi aliyekuwa na fikra na falsafa za dhana ya kujitegemea wakati wa uongozi wake.
Rais Samia amesema hayo leo wakati akihutubia katika Mdahalo wa Kitaifa wa kuadhimisha Miaka 100 ya Kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere mjini Kibaha mkoani Pwani.

Aidha, Rais Samia amesma, Mwalimu Nyerere aliamini Tanzania na Mataifa mengine ya Afrika hayawezi kuwa na nguvu ya kuijiamulia mambo yake endapo yataendelea kuwa na uchumi tegemezi hivyo hatuna budi kuwajibika kwa kuchapa kazi na kutumia vizuri rasilimali tulizonazo ili tujitegemee kiuchumi.

Rais Samia amesema, ili kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi, Serikali ya Awamu ya Sita inafanya jitihada mbalimbali kama kuimarisha huduma za afya, miundombinu ya elimu na viwango vya elimu.
Aidha, Rais Samia amemuelezea Mwalimu Nyerere kama kiongozi aliyejenga misingi imara ya amani, umoja, na mshikamano tuliyonayo hivi sasa ambayo inaendelezwa na kila awamu ya uongozi.

Rais Samia ametoa wito kwa Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Nyerere kuwa kitovu cha uandishi na uhifadhi wa historia ya harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika na maeneo yaliyohusishwa katika harakati za ukombozi yatambuliwe na kuendelezwa ili yatumike kama kivutio cha utalii wa kihistoria.
Katika maadhimisho hayo, Rais Samia alizindua vitabu vitatu ambavyo ni: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere: Chemchemi ya Fira za Kimapinduzi; Misingi ya Falsafa, Itikadi na Sera za Chama Cha Mapinduzi na Development as Rebellion chenye Juzuu Tatu za The Making of a Philosopher Ruler, Becoming Nationalist na Rebellion without Rebels.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali, wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wananchi wa Pwani katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Daniel Chongolo (kulia) wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa kuadhimisha miaka 100 ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani leo Aprili 9, 2022.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Mzee Joseph Butiku akimvisha Katibu Mtendaji wa Chama Cha Mapinduzi Mstaafu na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mstaafu Mzee Pius Msekwa (kulia) beji ya Maadhimisho ya Miaka 100 ya Mwalimu Julius Nyerere wakati wa Mdahalo wa Kitaifa wa kuadhimisha miaka 100 ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyika katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha mkoani Pwani leo Aprili 9, 2022.
Sehemu ya Viongozi mbalimbali wakifatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali, wanafunzi wa Vyuo Vikuu na wananchi wa Pwani katika Mdahalo wa Kitaifa wa Kumbukizi ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha Mkoani Pwani. (Picha na Ikulu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news