Vijiji 75 Arusha vyanufaika na uamuzi wa Rais Samia

NA MUNIR SHEMWETA-WANMM

JUMLA ya vijiji 75 vilivyokuwa na migogoro ya matumizi ya ardhi katika Mkoa wa Arusha vimenufaika na uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kwake kubaki maeneo yake kufuatia vijiji hivyo kuingia kwenye migogoro ya matumizi ya ardhi na maeneo ya hifadhi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula akizungumza na viongozi pamoja na watendaji wa mkoa wa Arusha wakati wa ziara ya Mawaziri wa Kisekta kupeleka mrejesho wa Uamuzi wa Baraza la Mawaziri juu ya utatuzi wa migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 tarehe 20 Aprili, 2022.

Mkoa wa Arusha unahusisha vijiji na mitaa 116 kati ya 975 vyenye migogoro ya matumizi ya ardhi na hifadhi, mashamba, ranchi, mapori ya akiba na vyanzo vya maji ambapo taarifa yenye mapendekezo ya utatuzi wake iliwasilishwa serikalini tarehe 23 Septemba 2019 na kutolewa uamuzi na Baraza la Mawaziri.

Katika taarifa hiyo ilipendekezwa vijiji 920 kati ya 975 vyenye migogoro ya matumizi ya ardhi nchini kubaki ingawa baadhi yake vitahusisha marekebisho ya mipaka kwa njia shirikishi na baadhi yake migogoro yake ilishatatuliwa.
Sehemu ya washiriki wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha kilichofanyika mkoani Arusha tarehe 20 Aprili, 2022.
Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde akizungumza katika kikao kati ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 Aprili, 2022.

"Vijiji na mitaa 116 Arusha kuachiwa vijiji 75 kubaki kwenye maeneo yake ni hisani ya kipekee na tunatakiwa tuiheshimu na tusiitumie vinginevyo kwa sanababu Mhe. Rais Samia alikuwa na uwezo wa kutaka kuviondoa, lakini ameridhia maeneo 75 kubaki," alisema Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula.

Akizungumza na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 Aprili, 2022 wakati wa ziara ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta mkoani humo, Dkt.Mabula alisema, sambamba na uamuzi wa serikali, uongozi wa mkoa utakuwa na jukumu la kusimamia mpango wa matumizi ya ardhi sambamba kudhibiti vyanzo na vichocheo vyote vya kuzalisha migogoro.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega akuzungumza wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 Aprili, 2022.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi akizungumza wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 Aprili, 2022.


"Natambua mkoa wa Arusha unazo changamoto nyingi zinazosababishwa na muingiliano wa matumizi ya ardhi lakini niwakumbushe kuweka utaratibu mzuri wa utekelezaji uamuzi wa serikali unaohusu migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 nchini,"alisema Dkt.Mabula.

Kwa upande wao, Mawaziri wa Wizara za Kisekta walihimiza umuhimu wa viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi chini kusimamia vyema utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri bila kuleta taharuki kwa wananchi sambamba na kuhakikisha maeneo ya hifadhi yanatunzwa.Niabu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Khamis Hamza Chillo akisisitiza jambo wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 Aprili, 2022.Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande akizungumza wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 Aprili, 2022.

‘’Kama Wizara ya Kilimo tupo katika mchakato wa kutunga sheria ya kilimo kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi kutenga na kubaini maeneo yaliyotengwa kwa shughuli za kilimo ili kuondoa migogoro ya ardhi,’’alisema Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega alisema, uzoefu unaonesha kuwa maeneo mengi yaliyoathirika na uvamizi ni ya mifugo na kusisitiza kuwa maeneo hayo ni ranchi zinazotumika pia kama ardhi ya akiba na kuweka wazi kuwa, hakuna namna yoyote maeneo hayo kutoonekana vichaka.Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Allan Kijazi akizungumza katika kikao kati ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 Aprili, 2022.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela akizungumza wakati wa kikao baina ya Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta iliyoongozwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Angeline Mabula na uongozi wa mkoa wa Arusha tarehe 20 Aprili, 2022.

Tayari Kamati ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta katika awamu ya pili ya kupeleka mrejesho wa maamuzi ya baraza la Mawaziri kuhusiana na migogoro ya matumizi ya ardhi katika vijiji 975 imeshatembelea mikoa ya Pwani, Morogoro, Tanga, Mara na Arusha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news