TRA,Facebook wakaa meza moja kuhusu kodi, Ufaransa iliwahi kushinda

NA DIRAMAKINI

TIMU ya wataalamu wa Kampuni ya META inayomiliki mitandao ya Facebookapp, Instagram pamoja na Whatsapp leo Aprili 21, 2022 imefanya mazungumzo ya awali na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu namna ya kutoza kodi katika huduma zao nchini.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Makao Makuu jijini Dar es Salaam.

Pande hizo mbili zimejadiliana kuhusu mambo mengi, lakini kubwa ni kwa namna gani ambavyo, META wanavyopaswa wao kulipa kodi kulingana na mapato wanayoyapata hapa Tanzania.
Mwaka 2019 wakati wa utawala wa Rais wa Marekani, Bw. Donald Trump alipendekeza ushuru wenye thamani ya dola bilioni 2.4 dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Ufaransa hususani mikoba ya wanawake, jibini ili kulipiza kisasi kwa Uraransa.

Ni baada ya Taifa hilo la Ulaya kutangaza kuyatoza kodi makampuni ya kidigitali kutoka Marekani ikiwemo Facebook kwa sasa Meta, Google na Amazon.

Wakati huo, Ofisi ya Mwakalishi wa Kibiashara wa Marekani ilisema kuwa, kodi mpya ya Ufaransa ilikuwa na thamani ya bidhaa za Ufaransa.

Hata hivyo, mwaka juzi kwa shingo upande, kampuni tanzu ya Facebook ya FB.O ya Ufaransa ilikubali kulipa zaidi ya Euro milioni 100 (dola milioni 118) kama kodi ya huko nyuma, ikiwa ni pamoja na adhabu, baada ya ukaguzi wa miaka 10 wa akaunti zake uliofanywa na mamlaka ya mapato ya Ufaransa.

Kampuni hiyo ilibainisha hayo kupitia taarifa iliyonukuliwa na mashirika mbalimbali ya habari za Kimataifa ikielezea kuhusiana na uamuzi huo.

Ufaransa nayo imekuwa ikijitahidi kurekebisha sheria za Kimataifa za ushuru kwenye kampuni za kidijitali kama vile Facebook (Meta), Google, Apple (AAPL.O) na Amazon (AMZN.O) kwani ilibaini kampuni hizo za kiteknolojia zilikuwa zinalipa ushuru mdogo sana nchini humo wakati wanafanya mauzo makubwa kupitia huduma zao.

Wakati huo, Msemaji wa Facebook alisema mamlaka ya ushuru ya Ufaransa ilifanya ukaguzi kwenye akaunti za Facebook katika kipindi cha 2009-2018, ambayo ilisababisha makubaliano na kampuni tanzu kulipa jumla ya Euro milioni 106.

Msemaji wa Facebook pia alisema kuwa, tangu 2018 kampuni hiyo imeamua kujumuisha mauzo yake ya matangazo nchini Ufaransa katika akaunti zake za kila mwaka zinazohusu biashara wanazofanya nchini Ufaransa.

Msemaji huyo wa Facebook hakufafanua zaidi kuhusu maelezo ya makubaliano hayo ikiwemo mamlaka inayoshughulika masuala ya kodi ncini humo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news