Wakubali kwa kauli moja Dodoma Jiji kushirikiana na Jiji la Nagai nchini Japan

NA DENNIS GONDWE

BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma limekubali kwa kauli moja maombi ya kuanzisha ushirikiano baina ya Jiji Nagai la Japan na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa manufaa ya wananchi wa pande mbili.
Akiwasilisha taarifa ya Mwenyekiti katika Mkutano wa kawaida wa Baraza la Madiwani, Mwenyekiti wa mkutano huo ambae pia ni Mshahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe alisema kuwa siku kadhaa zilizopita ofisi yake ilitembelewa na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Balozi Baraka Luvanda na kuwasilisha barua ya kuomba ushirikiano huo. 

“Madhumuni ya kuwasilisha taarifa hii ni kuomba ridhaa ya Baraza la Madiwani kuanza mazungumzo ya makubaliano ya ushirikiano huo. Aidha, tayari Jiji hilo limeonesha utayari wa kutoa gari la kubeba wagonjwa na gari la zimamoto na uokoaji kwa Jiji la Dodoma.

Baada ya maelezo hayo Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lilikubali kwa kauli moja kuanza hatua za awali za mazungumzo ya ushirikiano huo.
Jiji la Nagai lipo katika Jimbo la Yamagata likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 214.67, shughuli kubwa za kiuchumi zikiwa ni kilimo na viwanda vyepesi vya vifaa vya umeme na viwanda vya madawa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news