Wizara ya Maji yafikisha tabasamu Mangaka

NA DIRAMAKINI

WAKAZI wa mji wa Mangaka katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wana kila sababu ya kufurahi baada ya moja ya kisima cha maji safi kufika katika hatua za mwisho kupitia mradi wa kuboresha hali ya upatikanaji wa majisafi, salama na yenye kutosheleza kufika katika hatua za mwisho.
Utekelezaji wa mradi huo ni matokeo ya maelekezo ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga kuhusu kuimarisha hali ya huduma ya maji kwa wananchi katika eneo hilo.
Pichani ni viongozi na watendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Masasi-Nachingwea (MANAWASA), mamlaka inayotekeleza mradi huo katika mji wa Mangaka wakikagua miundombinu ya mradi katika hatua za mwisho za utekelezaji, Mtaa wa Mchangani.

Post a Comment

0 Comments