Askofu Mulilege Mkombo afukuzwa Tanzania tena, alitumia kimvuli cha dini kuishi bila kibali

NA DIRAMAKINI

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la House of Prayer Shield of Faith Christian Fellowship, Mulilege Mkombo (Mukombo Muyondi) maarufu zaidi kwa jina la Mzee wa Yesu amefukuzwa nchini Tanzania kwa kosa la kuhamia na kuishi bila kuwa na vibali vya kuishi.

Ni utaratibu ulio wazi kuwa, mgeni yeyote anayekusudia kuishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya uwekezaji, ajira au shughuli yoyote halali atapewa kibali cha mkazi.
Raia huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inadaiwa aliingia nchini Tanzania chini ya mwamvuli wa dini ambapo kufukuzwa kwake sasa kwa mara ya tatu.

Msemaji wa Uhamiaji, Paul Mselle amesema hilo limefanikishwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Ubalozi wa Jamhuri ya Kidemokria ya Congo nchini.

"Mara ya kwanza mtuhumiwa aliondoshwa nchini mnamo Februari 2, 2011, mara ya pili Agosti 28, 2019 na sasa leo Mei 24, 2022 baada ya kubainika yupo tena nchini mnamo Mei 15,2022,"amesema

Askofu Mulilega anarejeshwa nchini kwao kwa mujibu wa kifungu na 25 (2) (c)cha sheria ya uhamiaji sura ya 54 ya mwaka 2016.

Pia Mselle amewataka wananchi kutompokea kwenye familia, nyumba za ibada na kutoshirikiana nae kwa namna yoyote ile na atakayefanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news