Waziri Ndumbaro ataja faida ya sheria ya usuluhishi

NA DIRAMAKINI

UWEPO wa Sheria mpya ya Usuluhishi wa migogoro kwa njia mbadala nje ya Mahakama ni hatua kubwa katika kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini Tanzania.
Waziri Dkt.Damas Ndumbaro (wa nne kutoka kushoto) katika picha ya pamoja.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro ameyasema hayo leo Mei 24, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa siku tatu wa masuala ya haki na usuluhishi wa migogoro ya kibiashara barani Afrika kwa njia mbadala.

"Madhumuni makuu ya kupitishwa kwa Sheria ya Usuluhishi ni kuhimiza mbinu za utatuzi wa haraka wa migogoro bila kuingiliwa na mahakama” alisema Dkt. Ndumbaro

“Sheria ya usuluhishi tayari imepelekea kuanzishwa kwa Kituo cha Usuluhishi (Arbitration Centre) ambacho tunalenga kiwe bora na chenye hadhi ya kuaminika kimataifa” Alisema Dkt. Ndumbaro

Aidha, Dkt. Ndumbaro amesema ni ukweli usiopingika kwamba kutokana na ongezeko la uwekezaji na biashara, idadi ya migogoro ya kibiashara ni lazima izuke. hivyo ni bora kutumia njia mbadadala kwa utatuzi wa haraka, wa gharama nafuu na wa haki kwa migogoro ya kibiashara, kila inapowezekana.
Usuluhishi mbadala wa migogoro duniani umekuwa chombo kikuu cha utatuzi wa majukumu ya kimkataba. Uzoefu wa kawaida ni kwamba michakato mbadala ya utatuzi wa mizozo huhifadhi na kuimarisha uhusiano wa kibinafsi na wa kibiashara.

Faida za msingi za mfumo wa Usuluhishi Mbadala ni wenye utaratibu; gharama ya chini na huondoa haraka migogoro. Kwa hivyo utaweza kusaidia kutatua migogoro mingi ya kibiashara ya ndani na kimataifa kwa manufaa ya pande zote kwa ubora, kuliko mchakato wa kawaida wa kisheria

Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa Ujerumani, Dkt. Katrin Bornemann amesema Ujerumani kupitia Taasis yake ya GIZ itaendelea kushirikiana na Wizara ya Katiba na Sheria hususani eneo la kupata Haki kwa urahisi hasa wanawake na watoto.

Mwisho, Dkt. Ndumbaro amewashukuru GIZ kwa kutoa msaada wa kifedha na kiufundi katika mkutano huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news