Maagizo ya Waziri Bashungwa kwa wakuu wa mikoa kuhusu halmashauri

NA ANGELA MSIMBIRA, OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa wote nchini kuhakikisha wanazisimamia Mamlaka za Serikali za Mitaa ziweze kutumia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama ilivyopangwa.
Akifungua kikao kazi cha Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa leo Mei 24, 2022 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri, Naibu Waziri OR-TAMISEMI, Mhe.David Silinde amesema Wakuu wa Mikoa wanawajibu wa kusimamia utekelezaji wa Miradi ya maendeleo katika Ngazi za Halmashauri na kuhakikisha Halmashauri zinatekeleza majukumu yao kikamilifu.
Mhe. Silinde amewataka viongozi hao kuhakikisha wanafanya uchambuzi wa mahitaji halisi ya mashine za kukusanyia mapato (POS) ili waweze kufahamu mapungufu yaliyopo na kuchukua hatua stahiki, lengo likiwa ni kuhakikisha mashine hizo zinatumika katika ukusanyaji wa mapato.
Amewataka Wakuu wa Mikoa kuzisimamia Halmashauri pindi zinapoandaa makisio ya bajeti ya mapato ya ndani ili bajeti hiyo iendane na uhalisia na fursa zilizopo kwenye Halmashauri.

Mhe. Silinde pia amewataka Viongozi hao kuhakikisha wanazisimamia Halmashauri kujibu hoja zilizotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kaguzi nyingine ili hoja hizo ziweze kufungwa.

Pia amewaagiza Wakuu wa Mikoa wote kufanya maamuzi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa maslahi ya Mkoa na Taifa kwa ujumla na kuwachukulia hatua watumishi wanaokiuka maadili ya utumishi kwa kuzingatia sharia, miongozo na taratibu za Utumishi wa Umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news