Barrick yapeleka tabasamu Sekta ya Elimu Halmashauri ya Nyang’hwale

NA DIRAMAKINI

MPAGO wa Kuinua Ufaulu Shuleni (Performance Improvement Program (PIP) unaotekelezwa na Kampuni ya Barrick kupitia Mgodi wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Nyang’hwale iliyopo mkoani Geita, umefanikiwa kupata matokeo mazuri kwa kuongeza idadi ya ufaulu wa wanafunzi wilayani humo.
Baadhi ya walimu kutoka shule za sekondari zilizochangia kufanikiwa kwa mpango huu wakipokea zawadi za motisha kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale,Jamhuri David William.
Egide John Halalawe,kutoka sekondari ya Msalala aliyepata daraja la kwanza katika mtihani wa kidato cha nne mwaka jana akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale,Jamhuri David William.

Kabla ya kuanzishwa mpango huu unaolenga shule za sekondari ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne wilayani humo kwa kiwango cha daraja la kwanza ulikuwa wa wanafunzi watano kwa sasa idadi imeongezeka kufikia wanafunzi 55.

Hayo yamebainishwa wakati wa hafla ya kuwatunukia zawadi wanafunzi kutoka shule mbalimbali waliofaulu vizuri sambamba na walimu waliofanikisha ufaulu huo kupitia programu PIP.
Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale,Jamhuri David William akiendelea kuwatunza wanafunzi waliokuwa wakitoa burudani ya ngoma katika hafla hiyo.
Baadhi ya Walimu kutoka shule za sekondari zilizochangia kufanikiwa kwa mpango huu wakipokea zawadi za motisha kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale,Jamhuri David William.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika wilayani humo na kuhudhuriwa na Walimu, wazazi, wanafunzi na wafanyakazi wa Barrick alikuwa ni Mkuu wa wilaya hiyo,
Jamhuri David William. 

 Progamu hiyo ilianzishwa mwaka 2019 kwa lengo la kuinua kiwango cha ufaulu kwa Wanafunzi wa shule za Sekondari na kupunguza utoro mashuleni hususani kwa Wasichana. Kutokana na matokeo chanya ya mpango huu kwa wanafunzi, Kamati ya Maendeleo ya Jamii (CDC) ya imekuwa ikitenga fedha kila mwaka ili kufanikisha utekelezwaji wake.
Meneja wa Mahusiano ya Kijamii wa Barrick Bulyanhulu, Agapiti Paul akiongea kuhusu mafanikio ya mpango wa kuongeza Ufaulu. 

Meneja wa Mahusiano ya Kijamii wa Barrick Bulyanhulu, Agapiti Paul, alisema katika kipindi cha mwaka 2021 kampuni ilitenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwenye bajeti ya miradi ya Kijamii (CSR) katika Halmashauri ya Nyang’hwale, kwa ajili kununua vitabu kwa ajili ya wanafunzi na walimu katika shule 10 za sekondari za Serikali wilayani humo, kutoa zawadi za motisha kwa wanafunzi waliofaulu kwa daraja la kwanza, wazazi wa wanafunzi hao, walimu ambao masomo wanayofundisha wanafunzi waliyafaulu vizuri na shule ambazo zimepata wanafunzi wenye ufaulu huo.
Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale,Jamhuri David William akiongea katika hafla hiyo
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale, David Jamhuri, alipongeza jitihada zinazofanywa na Barrick kutoa motisha kwa walimu na wanafunzi kwa lengo la kuongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi wilayani humo.

”Ninaamini ushirikiano wa Serikali na Barrick kupitia mpango huu utaleta mafanikio makubwa zaidi, Natoa wito kwa walimu na wanafunzi kuongeza bidii wakati wote kufanikisha malengo ya Serikali ya kuboresha sekta ya elimu ya elimu nchini ambayo inazidi kuboresha miundo mbinu mashuleni na kukabili changamoto mbalimbali zilizopo,”alisema.
Mmoja wa wanafunzi aliyenufaika na mpango huu, Egide John Halalawe,kutoka sekondari ya Msalala akiongea kwa niaba ya wenzake alisema kupitia mpango huo wanafunzi wananufaika kwa kupata vitabu pia kupatiwa chakula shuleni na umewezesha walimu kufundisha kwa bidii na kusimamia kwa karibu wanafunzi wanapokuwa kwenye mwaka wa mtihani.

“Tunashukuru Barrick na Halmashauri kwa kubuni mpango huu, tuna imani utawezesha wanafunzi wengi kufanya vizuri zaidi katika mitihani yao ikiwemo kupata daraja la kwanza na madaraja mengine ya juu ya ufaulu,”alisema.
Picha ya pamoja ya watendaji wa wilaya,Barrick na walimu wakati wa hafla hiyo.

Akiongea kwa niaba ya wazazi, Idd John alisema, mpango huu ni mzuri na unahamasisha watoto kujituma zaidi pia wazazi wengi wasio na uwezo watoto wao wanasoma vizuri kutokana na kupatiwa vitabu vya kutosha.

Sambamba na kupatiwa chakula mashuleni vilevile walimu wamekuwa wakifundisha wanafunzi waliopo kwenye mwaka wa mtihani wakati wa vipindi vya likizo bila kuhitaji malipo yoyote kutoka kwa wazazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news