Waziri Mhandisi Masauni aagiza 'Panya Road' wasafishwe Dar

NA DIRAMAKINI

WAZIRI wa Mambo ya ndani, Hamad Masauni atoa maagizo kwa Jeshi la Polisi kuwakamata vijana wanaodhaniwa kuwa ni 'Panya Road' katika kata ya Zingiziwa, Mtaa wa Gogo na Chanika jijini Dar es Salaam.
Amelitaka Jeshi la Polisi nchini kuwakamata vijana wanaodhaniwa kuwa ni 'Panya Road' huku akiwaasa wazazi kuwa ndio walinzi namba moja juu ya watoto wao na katika familia zao.

Pia Mhandisi Masauni amewaasa wananchi wa Jimbo la Ukonga kuwa na ulinzi shirikishi katika maeneo yao. Amewaasa wananchi wa kata hizo kuwa na ushirikiano na Jeshi la Polisi katika eneo hilo ili kudhibiti uhalifu unaoendelea katika maeneo ya

Ameyasema hayo Mei 3, 2022 alipotembelea katika kata hizo na kusisitiza kuwa, vitendo vinavyofanywa na vijana hao havikubaliki kabisa katika jamii.

Aprili, 24, 2022 Jimbo la Ukonga katika Kata ya Chanika, Gogo na Zingiziwa kuliibuka kundi la vijana wanaojiita 'Panya Road' ambao waliwajeruhi wananchi kwa mapanga, kuvunja na kuiba vitu mbalimbali majumbani.

Post a Comment

0 Comments