Ujumbe wa Tanzania wateta na Mkurugenzi Mtendaji wa Africa-CDC jijini Geneva

NA OR-TAMISEMI, Geniva

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Grace Magembe leo Mei 24,2022 ameongoza ujumbe wa Tanzania katika kikao cha pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Afrika (Africa-CDC), Dkt. Ahmed Ogwell.
Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Geneva nchini Uswisi, Dkt.Grace amewasilisha hatua kubwa iliyopigwa na Serikali katika kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za kinga na tiba ili kuboresha huduma za afya nchini Tanzania.

Katika kikao hicho,Taasisi ya Africa-CDC wamesema wako tayari kushikiana na Tanzania katika kuimarisha ufuatiliaji na udhibiti wa magonjwa yasiyoambukiza (NCD) na yale ya kuambukiza, kuimarisha uwezo wa maabara ya Taifa na maabara za afya ya msingi katika utambuzi na ugunduzi wa magonjwa, vifaa na vifaa tiba.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt.Aifelo Sichalwe amewahakikishia Africa-CDC ushirikiano ndani ya Serikali na usimamizi wa rasilimali zote zitakazohusika kwenye afua zote.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news