Maandalizi ya Sensa 2022 yashika kasi, NBS yazikutanisha NGOs jijini Dodoma

NA DIRAMAKINI

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imekutana na Viongozi wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs) mkoani Dodoma kuzungumzia maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.
Akizungumza na washiriki wa mkutano huo, Kamisaa wa Sensa Mhe. Anne Makinda amesema NGOs ni wadau muhimu sana katika kufanikisha Sensa kwani wanafanyakazi na wananchi na wapo karibu na jamii.
“Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali ni wadau wakubwa sana katika kufanikisha Sensa ya Mwaka 2022. Ninyi kama viongozi wa NGOs, katika shughuli zenu za kila siku mkahamasishe wananchi washiriki kwenye Sensa ili Serikali ipate takwimu zitakazosaidia kupanga mipango ya maendeleo” amesema Kamisaa wa Sensa.

Kwa upande wake Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa amesema NGOs ni miongoni mwa makundi ambayo NBS itashirikiana nao kwa ukaribu ili kuhakikisha elimu ya umuhimu wa Sensa inawafikia wananchi wote.
Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Baraza la NGOs Dkt. Lilian Badi amesema Baraza la NGOs lipo tayari kutoa elimu ya Sensa na kuhakikisha kwenye shughuli za kila siku za wanachama, elimu ya Sensa inatolewa. Sensa ya Watu na Makazi itafanyika tarehe 23 Agosti, 2022. “Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa”

Post a Comment

0 Comments