PICHA:KIKAO KAZI CHA WATAALAM CHA KUKAMILISHA MPANGO WA KUJIANDAA NA KUKABILI MAAFA NA MKAKATI WA KUPUNGUZA VIHATARISHI VYA MAAFA WILAYA YA KYELA

Sehemu ya wajumbe wa kikao kazi cha kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya ya Kyela wakijadiliana wakati wa kazi za makundi.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. SACP Ismail Mlawa akihutubia wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wataalam wa Wilaya hiyo, kilicholenga kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa katika Wilaya hiyo Jijini Mbeya. Kikao kiliratibiwa na Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu na kufanyika tarehe 24 Mei, 2022.
Mwakilishi kutoka Taasisi ya SONGWECOM Bw. Ghoyela Mpangala akiwasilisha kazi ya kundi lake mara baada ya majadiliano wakati wa kikao kazi hicho.
Mjumbe wa Kamati ya Maafa Wilaya ya Kyela Bw. David Masanja (Afisa Kilimo) akiwasilisha kazi ya kundi lake mara baada ya majadiliano wakati wa kikao kazi hicho.
Mwakilishi kutoka Msalaba Mwekundu Kyela, Bw. Zawadi Jackson akiwasilisha kazi ya kundi lake mara baada ya majadiliano wakati wa kikao kazi cha kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya hiyo
Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally Mwatima akiwapitisha wajumbe wa kikao kazi hicho (hawapo pichani) wakati wa kuujadili Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Mwezeshaji kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Ally Mwatima akiwapitisha wajumbe wa kikao kazi hicho (hawapo pichani) wakati wa kuujadili Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya.
Afisa habari Wilaya ya Kyela Bw. Fredy Kabutu akiongoza kikao kazi cha Wataalam wa Wilaya hiyo, kilicholenga kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa katika Wilaya hiyo.
Mratibu wa Maafa Mkoa wa Mbeya Bw. Juma Maduhu akifafanua jambo wakati wa kikao kazi hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. SACP Ismail Mlawa (wa pili kulia waliokaa) pamoja na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi wa kikao kazi cha kukamilisha Mpango wa Kujiandaa na Kukabili Maafa na Mkakati wa Kupunguza Vihatarishi vya maafa Wilaya hiyo. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).

Post a Comment

0 Comments