Makachero wadaka 65 Pwani wakiwemo wezi wa miundombinu ya TANESCO

NA DIRAMAKINI

WATU 65 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za kukutwa na miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) huku thamani yake ikikadiriwa zaidi ya shilingi milioni 12.5.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo amesema kuwa watu hao walikamatwa wakati wa operesheni iliyofanyika kwa kipindi cha wiki tatu.

Lutumo amesema kuwa, watu hao walikamatwa kwa kushirikiana na TANESCO ambapo vitu hivyo viliibiwa kwenye miundombinu ya umeme.

"Watuhumiwa hao watano walitarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazowakabili za kuiba vifaa mbalimbali vya miundombinu ya umeme,"amesema Lutumo.

Ametaja vifaa hivyo kuwa ni Cooper waya zenye uzito wa kilogramu 429, transfa winding kilogramu 300, transfoma core kilogramu 32 na earth roads kilogramu 32.

"Wananchi wanapaswa kuishi kwa kufuata sheria na taratibu za nchi zilizowekwa na kitendo cha uhujumu miundombinu ya umeme ni hatari kwa maisha yao,"amesema Lutumo.

Katika hatua nyingine watu 60 walikamatwa kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kilogramu 15 na mbegu zake kilogramu tano, wizi na uvunjaji.

Amesema, watu 21 walifikishwa mahakamani huku wengine wakiendelea na uchunguzi juu ya matukio waliyoyafanya.

Aidha, alisema kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema katika kipindi cha Sikukuu ya Eid Al fitri kwa kuimarisha doria za magari, miguu na pikipiki ili wananchi washerehekee kwa amani.

Amewataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima ambazo huhatarisha maisha na uharibifu wa mali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news