MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA) YAZIDI KUBORESHA MIUNDO MBINU YA ELIMU DODOMA

NA ELIAFILE SOLLA-TEA

MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imeendelea kuboresha miundombinu ya Elimu jijini Dodoma kwa kuwezesha ukarabati na upanuzi wa shule nne za msingi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe akimuongoza, Prof. Maurice Mbago ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEA na ujumbe wake katika ukaguzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa Shule ya Msingi Kisasa.

Katika ufuatiliaji wa miradi mbalimbali inatotekelezwa na TEA, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Prof. Maurice Mbago ametembelea mradi wa utanuzi na ukarabati wa shule nne za Msingi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliofadhiliwa na TEA na kuridhishwa na utekelezaji wa mradi huo uliogharimu Sh. Bilioni 1.9.
Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Prof. Maurice Mbago, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bi. Bahati Geuzye wakikagua ukarabati na upanuzi wa Shule ya Msingi Medeli.

Katika ziara hiyo ya siku moja, Prof. Mbago, ametembelea Shule ya Msingi Medeli na Kisasa ambazo ni miongoni mwa shule nne zilizofadhiliwa na TEA.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Medeli, Bi.Grace Lisasi akitoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Prof. Maurice Mbago alipofanya ziara katika shule hiyo kukagua maendeleo ya mradi.

Shule nyingine zilizifadhiliwa ni Mlimwa C na Kizota.

Walimu wakuu wa Shule za Msingi Medeli Bi. Grace Lisasi na Shule ya Msingi Kisasa,Bi. Jesca Mwarabu wamesema mradi huo umesaidia kuongeza ufaulu na udahili wa wanafunzi
Prof. Maurice Mbago (mwenye bahasha) ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya TEA akifurahia jambo na Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe walipokutana katika ziara ya kukagua mradi shule Msingi Kisasa.

Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amepongeza TEA kwa ufadhili huo ambao amesema umeboresha mwonekano miundombinu na mandhari za shule nufaika
Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Bahati Geuzye amehimiza wanufaika wa mradi huo kutunza vizuri miundombinu hiyo kwa manufaa ya Watanzania.

Post a Comment

0 Comments