MAWAKILI WAVUTIWA NA UWEZO WA PROF.HOSEAH

NA DIRAMAKINI

BAADHI ya Mawakili na wadau wa sekta ya sheria nchini wamezungumzia uwezo wa mgombea urais Tanganyika Law Society (TLS), Prof. Edward Hoseah.
Wadau hao wameeleza kuridhishwa na uwezo wa kiuongozi aliouonyesha na kuwa anastahili nafasi hiyo kwa mara nyingine ili aweze kuendeleza na kuongeza kasi ya mabadiliko chanya ndani ya TLS.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau na mawakili hao wametoa wito kwa wapiga kura kumpigia kura Prof. Hoseah ili aweze kuiongoza TLS kwa awamu nyingine.Hatua kwa hatua wasikilize wadau katika video hizi fupi fupi;

"Profesa Hoseah amekuja na sera ya Constructive Engagement ambayo ni falsafa inayoleta mahusinano mema au inaimarisha mahusiano yaliyopo kati ya Tanganyika Law Society pamoja na wadau wake wakubwa, hususani Serikali, tunapoeleza kurejesha mahusiano mema kati ya Serikali ni kwamba mawakili tunahitaji kupata fursa mbalimbali zilizopo ndani ya nchi yetu na nje ya nchi"

 "Mimi ni mpiga kura halali ambaye ninashiriki katika chaguzi mbalimbali zikiwemo chaguzi za viongozi wakuu wa Chama cha Mawakili Tanganyika, kwa maana ya kwamba kwa nafasi ya Rais wa TLS, Makamu wa Rais,wajumbe wa baraza la uongozi la TLS pamoja na chaguzi nyingine ambazo zipo chini ya mwamvuli wa TLS. Kwenye uchaguzi huu ambao unakwenda kufanyika mwaka huu, mwezi huu pale Arusha. Tukizungumzia uchaguzi huu, mimi binafsi ninamuunga mkono mgombea Urais, anayejulikana kwa jina la Profesa Edward Hoseah...Ninaamini ataivusha TLS,ataisogeza TLS kutoka hapa tulipo kwenda sehemu nyingine"

 "Nimefuatilia uongozi wa Profesa Edward Hoseah,akiwa kama Rais wa Tanganyika Law Society,nimefurahiswa na mabadiliko ambayo ameweza kufanya akiwa kama Rais, ninategemea kipindi cha pili endapo atachaguliwa atafanya mambo makubwa zaidi hasa kutengeneza midahalo kati ya Serikali na Chama cha Wanasheria"

 "Profesa Edward Hoseah..nimefuatilia kampeni zake na uongozi wake ulivyoenda, kwa kweli ameturidhisha inaweza kuwa si kwa kiasi chote, lakini kwa namna fulani amefikia malengo aliyoahidi,na ninatumaini tukifanikiwa, na tukiweza kwa pamoja kumpa kura za ndiyo anaweza kufanya mambo makubwa zaidi kuliko aliyoyafanya katika mwaka mmoja uliopita"."Nimevutiwa na sera ya Profesa Edward Hoseah ya Constructive Engagement kwa maoni yangu, sera hii itatusaidia kukuza mahusiano kati ya TLS na wadau wote nchi nzima, yenye kuleta manufaa kwa wanachama wa TLS, hivyo ningepeda kutoa wito kwa wanachama wote TLS kumpigia kura Profesa Edward Hoseah".

SAFARI YA KITAALUMA

Profesa Hoseah mwaka 1985 alitunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, akishinda pia Tuzo ya Mwanafunzi Bora ya Kitivo cha Sheria katika "Constitution Law".

- Mwaka 1989 alitunukiwa Shahada ya Uzamili katika Sheria (LLM) ya Chuo Kikuu cha Queens, Ontario, nchini Canada na kupewa Tuzo ya Mwanafunzi Bora ya Chuo Kikuu cha Queens.

- Mwaka 2007 alitunukiwa Shahada ya Uzamifu (PhD) katika Sheria ya Chuo kikuu cha Dar es salaam akibobea katika "Law of Evidence".

- Mafunzo katika Sera, Uongozi, Maadili na Kukabiliana na Rushwa katika Vyuo na Taasisi zifuatazo; Chuo Kikuu cha Passau (2007), Chuo kikuu cha Birmingham (2003) na Taasisi ya Benki ya Dunia (WI) mwaka 1998.

- Mwaka 1997 alihitimu Astashahada ya Utatuzi wa Migogoro kutoka katika Kituo cha Diplomasia (CFR) nchini Tanzania.

UZOEFU NA UBOBEZI KATIKA SHERIA

- Mhadhiri katika kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam ( Law of Evidence and Legal Practice)

- Mhadhiri katika Kituo cha Diplomasia (CFR) akifundisha Sheria katika Biashara za kimataifa na uwekezaji.

- Mwanazuoni (Visiting Scholar) katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Northwestern, Chicago (2003-2005)

- Profesa wa muda (Adjunct Professor) wa Shule ya Sheria ya Duke Nchini Marekani (2010 - 2012).

- Tuzo kutoka katika Taasisi ya kimataifa kwa mchango katika maboresho ya Sheria ya Jinai (2003).

- Wakili na Mkurugenzi katika Hosea & Co Advocates wabobezi na watoa huduma mbalimbali za kisheria.

- Mkufunzi wa Taasisi ya "Uongozi Institute" kuanzia mwaka 2019

- Profesa katika Chuo Kikuu cha Iringa kuanzia mwaka 2021

- Mwandishi wa vitabu na machapisho ya kitaaluma.

- Mjumbe wa Bodi mbalimbali na mshauri wa masuala ya kitaalam katika mawanda ya Sheria.


UZOEFU KATIKA SHUGHULI ZA UONGOZI

- Rais wa sasa wa Tanganyika Law Society (TLS) kuanzia mwaka 2021.

- Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania.

- Rais wa Mamlaka ya Kukabiliana na Rushwa Afrika Mashariki (2008-2010, 2014-2015).

- Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kukabiliana na Rushwa katika Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika-SADC ( SAFAC) mwaka 2010-2011.

- Mwenyekiti wa Bodi ya Umoja wa Afrika (AU) katika Mapambano ya Rushwa (2011-2012)

- Makamu wa Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Kukabiliana na Rushwa (IAACA, 2012-2015).

Post a Comment

0 Comments