'Mazoezi ni tiba ya magonjwa yasiyoambukiza'

NA DIRAMAKINI

IMEELEZWA baadhi ya watu wamekuwa wakisumbuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kutokana na kutofanya mazoezi.

Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Shangwe Twamala ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani wakati wa mazoezi ya pamoja ya kila mwisho wa mwezi kwa watumishi mbalimbali wa Serikali, mashirika ya umma, binafsi na wananchi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Pwani wakati wa mazoezi ambayo hufanyika kila mwisho na kuwa watu wanapaswa kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Twamala alisema kuwa, baadhi ya watu wamepata athari kubwa za kiafya kutokana na kutotenga muda wa kufanya mazoezi na kujikuta wakiathirika na magonjwa hayo na kwa vijana wataibua vipaji vyao.

Alisema, usipofanya mazoezi kuna athari nyingi za kiafya ikiwa ni pamoja na kupata magonjwa hayo yasiyo ya kuambukiza yakiwemo ya moyo, presha, uzito kupita kiasi na mengineyo hivyo ni vema watu wakashiriki michezo na kupata wachezaji wa michezo mbalimbali.

Aidha, alisema kuwa magonjwa hayo yameleta athari kubwa ndani ya jamii ikiwa ni pamoja na gharama kubwa za matibabu na kusababisha familia kuyumba kiuchumi pia husababisha hata vifo.

Kwa upande wake ofisa michezo wa mkoa wa Pwani, Grace Bureta alisema kuwa mazoezi hayo hufanyika kila mwisho wa mwezi ambapo hushirikisha watumishi na wananchi.

Bureta alisema kuwa mazoezi hayo ni utekelezaji agizo la serikali ambapo viongozi mbalimbali wa mkoa hushiriki na limekuwa na mafanikio makubwa kwani watu wengi hujitokeza na imekuwa njia mojawapo ya kuibua vipaji vya vijana.

Naye mwenyekiti wa Chama Cha Wauguzi Tanzania (TANNA) Mkoa wa Pwani Veronica Makange alisema walifanya mazoezi ya pamoja ambapo walikimbia umbali wa kilometa nane.

Makange alisema mazoezi ni muhimu kiafya kwani huuweka mwili vizuri na hata vyakula watu wanavyokula vinafanya kazi vizuri mwilini na kujiepusha na magonjwa yasiyoambukiza.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha (KEC) yalipofanyika mazoezi hayo Sixbert Luziga alisema kuwa eneo lao lina kila aina ya mchezo hivyo wananchi wanakaribishwa kutumia viwanja hivyo kufanya mazoezi.

Ruziga alisema wanaruhusu watu kufanya mazoezi kwenye viwanja hivyo ili watu waboreshe afya zao na kwa vijana waweze kuendeleza vipaji vyao ili kupata timu bora za baadaye.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news