Unajua kwamba Serikali ikifahamu idadi ya wananchi inarahisisha kutoa huduma, miradi ya maendeleo? Tujiandae Kuhesabiwa Agosti 23

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Septemba 14, 2021 jijini Dodoma alizindua rasmi Mkakati wa Uelimishaji na Uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Rais Samia alisema, lengo la mkakati huo ni kupata taarifa sahihi za idadi ya watu waliopo nchini ikiwemo jinsia, elimu, afya na hali za ajira ili kuwa na takwimu sahihi zitakazoiwezesha Serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa ajili ya watu wake.

“Taarifa za Sensa zitatusaidia kujua idadi ya watu wapi walipo, elimu zao, afya zao, hali ya ajira zao pamoja na makazi yao, pia zitatusaidia kujua ongezeko la watu wetu ili tuandae Sera ya Taifa na kujua mgawanyo wa rasilimali kwa uwiano sawa kwa wananchi wetu,”alisisitiza Rais Samia.

Aidha, Rais Samia alisema, haiwezekani kupeleka huduma kwa wananchi wa eneo fulani kama haijulikani idadi ya watu katika eneo husika ambapo amewataka wananchi wote wakaolala ndani ya mipaka ya Tanzania usiku wa kuamkia siku ya sensa kushiriki zoezi hilo. Kwa pamoja Tujiandae Kuhesabiwa ifikapo Agosti 23, 2022.

Post a Comment

0 Comments