MJUE PROF. EDWARD HOSEAH MBOBEZI WA SHERIA ALIYEJITOA KUITUMIKIA TANGANYIKA LAW SOCIETY (TLS)

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambaye anatetea kiti chake, Profesa Edward Hoseah ni kati ya viongozi ambao wamefanikiwa kushirikiana na wenzake kuiendesha taasisi hiyo kwa mafanikio makubwa ndani ya mwaka mmoja.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 27, mwaka huu jijini Arusha, ambapo tayari kampeni za wagombea urais zimeanza tangu Aprili 15, mwaka huu na zinatarajiwa kuhitimishwa Mei 26, mwaka huu siku ambayo pia utafanyika uchaguzi katika nafasi nyingine ikiwemo ya viongozi wa kanda.

Kwa nini umchague Prof.Edward Hoseah?

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambaye anatetea kiti chake, Profesa Edward Hoseah ni kati ya viongozi ambao wamefanikiwa kushirikiana na wenzake kuiendesha taasisi hiyo kwa mafanikio makubwa ndani ya mwaka mmoja.

Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kuishawishi Mahakama Kuu ya Tanzania kurejeshewa tozo ya shilingi milioni 450 ambazo tangu Uhuru walikuwa wakilipa mahakama kama ada.

Pia kupitia uongozi wake amefanikiwa kupunguza ada ya uwakili kutoka shilingi 60,000 hadi shilingi 20,000, kupunguza gharama ya afya kutoka shilingi milioni 1,050,000 hadi shilingi 500,000, kuimarisha uhusiano baina ya taasisi hiyo na Serikali ambao umeonesha nuru kubwa na mengineyo mengi.

Licha ya uzoefu mkubwa katika uongozi na ubobezi wa kutosha katika sheria, Profesa Hoseah ni miongoni mwa Watanzania wanaoipenda TLS, anaamini kupitia uongozi wake kwa kushirikiana na wenzake wanaweza kuistawisha zaidi taasisi hiyo muhimu.

SAFARI YA KITAALUMA

-Mwaka 1985 Alitunukiwa shahada ya kwanza ya Sheria (LLB) ya Chuo kikuu cha Dar es salaam, akishinda pia Tuzo ya Mwanafunzi bora ya Kitivo cha Sheria katika "Constitution Law".
- Mwaka 1989 Alitunukiwa shahada ya uzamili katika sheria (LLM) ya Chuo Kikuu cha Queens, Ontario, nchini Canada na kutupewa Tuzo ya Mwanafunzi bora ya Chuo Kikuu cha Queens.

- Mwaka 2007 Alitunukiwa shahada ya Uzamifu(PhD) katika Sheria ya Chuo kikuu cha Dar es salaam akibobea katika "Law of Evidence".

- Mafunzo katika Sera, Uongozi, Maadili na Kukabiliana na Rushwa katika Vyuo na Taasisi zifuatazo; Chuo kikuu cha Passau (2007), Chuo kikuu cha Birmingham (2003) na Taasisi ya Benki ya Dunia (WI) mwaka 1998.

- Mwaka 1997 Alihitimu Astashahada ya Utatuzi wa Migogoro kutoka katika Kituo cha Diplomasia (CFR) nchini Tanzania.

UZOEFU NA UBOBEZI KATIKA SHERIA

- Mhadhiri katika kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu Cha Dar es salaam ( Law of Evidence and Legal Practice)

- Mhadhiri katika Kituo cha Diplomasia (CFR) akifundisha Sheria katika Biashara za kimataifa na uwekezaji.

- Mwanazuoni (Visiting Scholar) katika Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Northwestern, Chicago (2003-2005)

- Profesa wa muda (Adjunct Professor) wa Shule ya Sheria ya Duke Nchini Marekani (2010 - 2012).

- Tuzo kutoka katika Taasisi ya kimataifa kwa mchango katika maboresho ya Sheria ya Jinai (2003).

- Wakili na Mkurugenzi katika Hosea & Co Advocates wabobezi na watoa huduma mbalimbali za kisheria.

- Mkufunzi wa Taasisi ya "Uongozi Institute" kuanzia mwaka 2019

- Profesa katika Chuo Kikuu cha Iringa kuanzia mwaka 2021

- Mwandishi wa vitabu na machapisho ya kitaaluma.

- Mjumbe wa Bodi mbalimbali na mshauri wa masuala ya kitaalam katika mawanda ya Sheria.

UZOEFU KATIKA SHUGHULI ZA UONGOZI

- Rais wa sasa wa Tanganyika Law Society (TLS) Kuanzia mwaka 2021.

- Mkurugenzi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana Rushwa (TAKUKURU) nchini Tanzania.

- Rais wa Mamlaka ya kukabiliana na rushwa Afrika mashariki (2008-2010, 2014-2015).

- Mwenyekiti wa Mamlaka ya kukabiliana na Rushwa katika nchi za SADC ( SAFAC) Mwaka 2010-2011.

- Mwenyekiti wa Bodi ya Umoja wa Afrika (AU) katika Mapambano ya Rushwa(2011-2012)

- Makamu wa Rais wa Taasisi ya kimataifa ya kukabiliana na rushwa (IAACA, 2012-2015).

Post a Comment

0 Comments