Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Mei 25,2022

NA GODFREY NNKO

LEO Won ya Korea Kusini (KRW) inanunuliwa kwa shilingi 1.81 na kuuzwa kwa shilingi 1.83 huku Dinar ya Kuwait (KWD) ikinunuliwa kwa shilingi 7486.4 na kuuzwa kwa shilingi 7550.9.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Mei 25, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Aidha, Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.6 na kuuzwa kwa shilingi 2.8 huku Metical ya Msumbiji (MZM) ikinunuliwa kwa shilingi 35.3 na kuuzwa kwa shilingi 35.6.
Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 343.3 na kuuzwa kwa shilingi 346.3 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 17.9 na kuuzwa kwa shilingi 18.1.

Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.60 na kuuzwa kwa shilingi 0.63 huku Franka ya Ubelgiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.10 na kuuzwa kwa shilingi 50.54.

Kwa upande wa Paundi ya Uingereza (GBP) inanunuliwa kwa shilingi 2859.05 na kuuzwa kwa shilingi 2888.6 huku Dola ya Marekani (USD) ikinunuliwa kwa shilingi 2288.9 na kuuzwa kwa shilingi 2311.8.

Aidha, Euro ya Ulaya (EUR) inanunuliwa kwa shilingi 2450.9 na kuuzwa kwa shilingi 2475.9 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 10.8 na kuuzwa kwa shilingi 11.5.

Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini (ZAR) inanunuliwa kwa shilingi 145.3 na kuuzwa kwa shilingi 146.8 huku shilingi ya Kenya (KES) ikinunuliwa kwa shilingi 19.6 na kuuzwa kwa shilingi 19.8.
Franka ya Rwanda (RWF) inanunuliwa kwa shilingi 2.22 na kuuzwa kwa shilingi 2.28 huku Franka ya Burundi (BIF) ikinunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news