MZFA YARIDHISHWA YA MABORESHO YA UWANJA WA CCM KIRUMBA

NA FABIAN FANUEL

MWENYEKITI wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA),Vedastus Lufano leo amefanya ukaguzi wa mwisho kupeleka mechi ya Ligi kuu baina ya Geita Gold FC vs Simba SC.
Akizungumzia maendeleo ya Uwanja, Lufano amesema Uwanja wa CCM Kirumba uko tayari kutumika katika mechi zote zilizopangwa na TFF kupitia Bodi ya Ligi TPLB ambazo ni Geita Gold vs Simba, Biashara United vs Yanga (Ligi kuu) na Yanga SC vs Simba SC (Azam Sports Federation Cup).

"Kwanza niwashukuru wamiliki wa uwanja kwa maboresho waliyoyafanya katika uwanja huu, wamefanya kazi kubwa na sisi kama MZFA tunawapongeza sana, hakika Uwanja umekuwa mzuri sana mechi yoyote hapa inachezeka vizuri bila shida"

"Pia nikipongeze kikosi kazi kutoka MZFA kikiongozwa na Katibu Mkuu MZFA Leonard Malongo kwa kazi kubwa waliofanya kwa kushirikiana na wamiliki wa Uwanja, wamefanya kazi kubwa ambayo wanastahili pongezi hizi,"amesema Vedastus Lufano.

Aidha, Lufano ameipongeza TFF chini ya Rais wake Mheshimiwa Wallace Karia kwa kuleta mchezo wa Nusu Fainali wa Azam Sports Federation Cup baina ya Yanga SC dhidi ya Simba SC, mchezo ambao unasubiriwa na watu wengi Tanzania na nje ya nchi.

"Kama MZFA tunamshukuru Rais Karia kwa kazi kubwa ambayo anayoifanya kwa ushirikiano mzuri na wasaidizi wake wote, wanafanya kazi nzuri na inapaswa kupongezwa na Watanzania wote. Sisi MZFA tunashukuru kwa nafasi ya kuleta mechi hii Mwanza, hakika tumepewa heshima na heshima hii tutailinda kwa nguvu zote," amesema Vedastus Lufano.

Mwenyekiti Lufano amefanya ukaguzi ya mwisho kuelekeaa mechi ya Jumapili Geita Gold FC dhidi ya Simba. Ukaguzi huo ukiwa umetanguliwa na ukaguzi aliyofanya Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidau na kisha Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Wallace Karia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news