NAIBU WAZIRI WA MADINI WA ZIMBABWE KUFANYA ZIARA HAPA NCHINI

NA MWANDISHI WETU

LEO Mei 23, 2022 Naibu Waziri wa Madini hapa nchini Dkt. Steven Kiruswa atampokea Naibu Waziri wa Madini wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Polite Kambamura na ujumbe wake kwa ziara ya siku tano.
Lengo la ziara hiyo ni kujifunza masuala mbalimbali ya usimamizi wa Sekta ya Madini kama utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na biashara ya madini.

Aidha, ujumbe kutoka Zimbabwe utajifunza kuhusu fursa ya madini yaliyopo Tanzania, mfumo wa usimamizi wa leseni Tanzania na usimamizi wa wachimbaji wadogo.

Pia, watatembelea mgodi wa dhahabu wa GGM na mtambo wa kusafisha dhahabu wa Mwanza, wachimbaji wadogo wa Nyarugusu ,na wachimbaji wadogo wa madini ya almasi Shinyanga.

Taarifa zaidi itawasilishwa wakati wa ziara hiyo hapa nchini

Post a Comment

0 Comments