Namungo FC yaichapa Biashara United 2-1

NA DIRAMAKINI

WANAJESHI wa Mpakani kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Musoma mkoani Mara, Biashara United imeshindwa kuonesha ubabe kwa Namungo FC kutoka mkoani Lindi.

Ni baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-0 katika mtanange wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliopigwa katika Dimba la Nyamagana jijini Mwanza.

Shiza Ramadhani Kichuya dakika ya tisa na 67 wa Namungo FC ndiye aliyesababisha maumivu kwa Biashara United.

Huku bao moja la Biashara United likifungwa na Ambroce Awio dakika ya 85 ya mtanange huo ambao ulikuwa wa kuvutia.

Kwa matokeo hayo, Namungo FC inafikisha alama 26 na kupanda nafasi ya tatu, ikiizidi alama mbili Geita Gold baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Biashara United inabaki na alama zake 23 za mechi 24 sasa ikishukia nafasi ya 13.

Post a Comment

0 Comments