Rais Samia afanya uteuzi Benki Kuu,Ranchi za Taifa na Shirika la Posta

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Viongozi kama ifuatavyo:-
Amemteua Bi. Sauda Kassim Msemo kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi huu, Bi. Sauda alikuwa Kamishna wa Fedha za Nje, Wizara ya Fedha na Mipango. Bi. Sauda anachukua nafasi ya Dkt. Bernard Yohana Kibesse ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Uteuzi huu unaanza tarehe 01 Juni, 2022.

Amemteua Mhandisi Cyprian John Luhemeja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO). Mhandisi Luhemeja ni Mtendaji Mkuu, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA).

Amemteua Bwana Macrice Daniel Mbodo kuwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC). Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mbodo alikuwa Kaimu Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania (TPC).

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Post a Comment

0 Comments