Rais Samia aomboleza kifo cha Askofu Charles Katale

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameelezea kupokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Ziwa Tanganyika la Kanisa la Moravian nchini, Askofu Charles Katale.
Mheshimiwa Rais Samia ameyabainisha hayo kupitia taarifa ya pole aliyoitoa kwa familia, ndugu jamaa na marafiki kupitia ukurasa wake rasmi wa Twitter leo Mei 4,2022.

"Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha aliyekuwa Askofu wa Jimbo la Ziwa Tanganyika la Kanisa la Moravian nchini, Askofu Charles Katale. Pole kwa Askofu Kiongozi Conrad Nguvumali, familia, waumini, ndugu, jamaa & marafiki. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina,"ameeleza Mheshimiwa Rais Samia.

Post a Comment

0 Comments