Rais Samia apokea tuzo ya mjenzi mahiri ya Babacar Ndiaye

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepokea tuzo ya Babacar Ndiaye (2022) kwa mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 kutoka kwa Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor kwa niaba ya Rais wa Benki hiyo Dkt. Akinumwi Adesina. Hafla ya Utoaji wa Tuzo hiyo imefanyika kwenye siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa AfDB, Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022.

Tuzo hiyo alipokea katika Mkutano wa 57 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) ambayo hupewa viongozi wa Afrika walio mstari wa mbele katika kuendeleza miundombinu.

Katika hafla hiyo, Rais Samia ametoa wito kwa nchi za Afrika kuungana, kuzijenga na kuziwezesha jumuiya za kiuchumi za kikanda na bara zima kwa ujumla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akionesha Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara, mara baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor tarehe 25 Mei 20220 Accra nchini Ghana.

Rais amesema lengo la ujenzi wa miundombinu Tanzania ni kuunganisha nchi, ukanda wa Afrika Mashariki na nchi za SADC ili kufikia agenda ya utangamano wa Afrika kiuchumi na kijamii.

Wakati huo huo, Rais Samia amesema ni lazima Afrika izalishe, ichakate na ifanye biashara ndani ya bara ili Soko Huru la Bara la Afrika (AfCFTA) liweze kutimiza malengo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor pamoja na viongozi mbalimbali wa Benki hiyo mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza katika siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) tarehe 25 Mei, 2022 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Accra, Ghana mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na Mafanikio yake kwenye Ujenzi wa Barabara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor pamoja na viongozi mbalimbali wa Benki hiyo mara baada ya kukabidhiwa Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 (Babacar Ndiaye Trophy 2022) kutokana na mafanikio kwenye Ujenzi wa Barabara. (Picha na Ikulu).

Vile vile, Rais Samia amesema maendeleo ya miundombinu ni mchakato endelevu, hivyo anatambua michango ya Marais waliotangulia katika ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini kupitia Mfuko wa Barabara na Taasisi za kifedha za kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news