SERIKALI KUWEKEZA ZAIDI KWENYE ELIMU NA UTAFITI WA TIBA-WAZIRI MKENDA

NA MATHIAS CANAL

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mheshimiwa Prof.Afolf Mkenda amesema, Serikali imedhamiria kuwekeza zaidi kwenye elimu ya utafiti na tiba.
Huo ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 na mpango mkakati wa serikali kupitia bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2022/2023 ambapo imepanga kutoa motisha kwa wahadhiri kutoka chuo chochote cha serikali ama binafsi akiweza kuchapisha andiko lake kwenye majarida ya juu, serikali itampa Shilingi milioni hamsini.

Waziri Mkenda ameyasema hayo tarehe 14 Mei 2022 wakati wa siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa LUPUS TANZANIA iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Jijini Dar es salaam.
Waziri Mkenda mesema kuwa kwa jumla yake serikali imetenga Bilioni moja kwa ajili ya wahadhiri hao na kufanya hivyo serikali inalenga kujenga uhusiano na uwezo zaidi kwa watafiti ili kuimarisha kipato chao jambo litakalowafanya waweze kufanya utafiti wakati wote na kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Amesema kuwa serikali itawawezesha wanafunzi wote ikiwemo kuwasomesha katika vyuo vikuu kwa wale watakaofaulu kwa kiwango cha juu kwenye masomo ya Sayansi.
Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo hicho,Prof. Andrea Pembe amesema kuwa serikali imeweka kipaumbele kwenye magonjwa mbalimbali ikiwemo uraibu wa dawa za kulevya na magonjwa ya kina mama yatokanayo na ujauzito, hivyo kuwepo kwa huduma hiyo nchini kumerahisisha kuwahudumia wananchi kwa kuwapatia tiba kirahisi wagonjwa ikiwa ni pamoja na upatikanaji kwa urahisi wa dawa japo gharama za dawa bado ni kubwa sana.
Prof.Pembe amesema kuwa katika tafiti zilizofanyika kwenye ugonjwa wa Lupus zinaonyesha watu wa asili ya Afrika ndio waathirika wakubwa na inakadiriwa watu 70-100 wanaathirika na ugonjwa wa Lupus kati ya watu 100,000.

Waziri Mkenda ameongeza kuwa,wanawake ndio wanaathirika zaidi na ugonjwa huo kwa uwiano wa wanawake 10 kwa mwanaume mmoja.
Aidha katika utafiti uliofanyika katika hospitali ya Taifa kutambua watoto waliokuwa na magonjwa b kwa kipindi cha miaka 7 (2012-2019) ulitambua watoto 52 waliokuwa na hayo magonjwa na miongoni mwao watoo 8 ambao ni sawa na asilimia 15% walikuwana ugonjwa wa Lupus.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news