SERIKALI YAHIMIZA USHIRIKISHWAJI ZAIDI ANUANI ZA MAKAZI

NA MWANDISHI WETU

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya amehimiza Ofisi za Umma na Ofisi Binafsi kuweka anuani za makazi katika majengo ya Ofisi zao ili kuwa mfano kwa wananchi wengine. 

Anuani hizo zitasadia kuonesha jina la ofisi yenyewe, mtaa iliyopo na eneo ambalo posti kodi hiyo ipo.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akizungumza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani katika ziara yake kukagua utekelezaji wa zoezi la anuani za makazi katika Mkoa wa Pwani.

Naibu Katibu Mkuu Mmuya amesema hayo katika ziara yake mkoani Pwani tarehe 13, Mei 2022 alipotembelea na kupokea taarifa ya Mkoa ya utekelezaji wa Anuani za makazi. 

Kwa sasa ngazi ya Taifa tumefikia asilimia 90 ya matarajio yetu,lakini tunazidiana Mkoa na Mkoa.

Amepongeza Mkoa wa Pwani kwa kutekeleza vyema zoezi la uwekaji wa anuani za makazi na kufuata miongozo iliyowekwa katika utekelezaji wa anuani za makazi.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya akiangalia kibao cha anuani za makazi kilichowekwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

“Ziara imelenga kujionea uhalisia ili mwezi huu, tutumie kurekebisha dosari chache tulizogundua kwa kupokea taarifa kwenye mfumo au kwa ziara mbalimbali tunazozifanya au taarifa tunazopatiwa alisema, Naibu Katibu Mkuu Mmuya,”amesema.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwn. Kaspar akipokea taarifa ya utekelezaji wa anuani za makazi ya Mkoa wa Pwani kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tehama Bwn. Ramadhani Mbura, (aliyesimama) kujionea utekelezaji wa zoezi hilo.

“Zoezi la anuani ya makazi ni endelevu, kila mmiliki mwenye eneo ambalo limejengwa au halijajengwa anapaswa kuwa na namba,alisema Naibu Katibu Mmuya”. Hiyo itasaidia kujua mahali eneo lilipo, wananchi wanahitaji kuelimishwa zaidi juu ya umuhimu wa zoezi la uwekaji wa anuani za makazi na itaongeza dhana ushirikishwaji wa wananchi.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bw. Yona Mwakilembe, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bwn. Kaspar Mmuya mara baada ya kuwasili kwa ajili kujionea utekelezaji wa zoezi la anuani za makazi katika Mkoa wa Pwani.

Akihitimisha Kaimu Meneja wa TANRODS Mkoa wa Pwani, Mhandisi Heririsper Mollel amesema utekelezaji wa anuani za makazi umefika katika hatua nzuri ukamilishaji wake kwa sasa wamejikita katika kurekebisha vibao vilivyokosewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news