Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Mei 30,2022

NA GODFREY NNKO

LEO shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.6 na kuuzwa kwa shilingi 19.8 huku Pula ya Botswana (BWP) ikinunuliwa kwa shilingi 190.23 na kuuzwa kwa shilingi 192.59.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Mei 30, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.59 na kuuzwa kwa shilingi 0.62 huku Franka ya Ubelgiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.11 na kuuzwa kwa shilingi 50.55.

Aidha,Won ya Korea Kusini (KRW) inanunuliwa kwa shilingi 1.83 na kuuzwa kwa shilingi 1.84 huku Dinar ya Kuwait (KWD) ikinunuliwa kwa shilingi 7493.6 na kuuzwa kwa shilingi 7558.1.

Aidha, Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.08 na kuuzwa kwa shilingi 2.24 huku Metical ya Msumbiji (MZM) ikinunuliwa kwa shilingi 35.3 na kuuzwa kwa shilingi 35.6.

Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 341.9 na kuuzwa kwa shilingi 345.1 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 18.04 na kuuzwa kwa shilingi 18.22.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news