Vijana chipukizi CCM wamegewa mbinu za kufikia ndoto zao

NA SHEILA KATIKULA

VIJANA Chipuziki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kutumia vizuri fursa ya elimu bure kwa kusoma kwa bidii ili kuweza kufikia nyanja za uongozi na kuhudumia taifa.
Vijana chipuziki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kongamano la UVCCM mkoani Mwanza.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Chipuziki Taifa, Yussuf Khashmir Haji wakati akizungumzana na chipuziki kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mwanza kwenye kongamano la Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) lililoandaliwa na chama.

Amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu anaendelea kufanya juhudi kubwa kutafuta pesa kwa ajili ya kuendeleza miradi ya elimu bure na ndiyo maana hivi karibuni ameshiriki kuigiza na kuzindua filamu ya Royal Tour ambayo inalenga kuhamasisha utalii.
Mwenyekiti wa Chipuziki Taifa, Yussuf Khashmir Haji.

Hata hivyo, aliongeza kuwa, kupata elimu kutasaidia kujiepusha na vitendo viuovu ikiwemo matumizi ya dawa za kulenya na uhalifu.

Aidha, ameiomba jumuia ya wazazi kuwalea chipuzikizi katika maadili mema ili waje kuwa viongozi wazuri wa chama siku za mbeleni.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Wilaya ya Ukerewe (UWT), Neema Mgobella amewasisitiza Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapundizi kuwaongoza vizuri chipukizi hao ili waje kushika nafasi ndani ya UVCCM na baadaye ngazi ya Jumuiya ya Wazazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news