Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu wakutana, Waziri Mhagama asisitiza jambo

NA JAMES K.MWANAMYOTO

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema ofisi yake inafanya kikao kazi cha siku mbili na Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ili kutathmini utendaji kazi kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama (hayupo pichani) alipokuwa akifungua kikao kazi cha siku mbili cha watumishi hao kilichoanza leo jijini Dodoma.

Mhe. Jenista ameyasema hayo Mei 26,2022 alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kufungua kikao kazi hicho kilichoanza jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Mhe. Jenista amesema ofisi yake imeamua kufanya kikao kazi hicho na watendaji hao kwani ndio wenye dhamana ya kusimamia rasilimaliwatu katika sekta zote za umma nchini kwa ajili ya ustawi wa taifa.

“Tukiongozwa na maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, nimeona nikutane na wasimamizi hao wa rasilimaliwatu kwa mara ya kwanza ili kuweka msingi wa kutathmni utendaji kazi katika utumishi wa umma ambao utatuwezesha kujitathmini kwa lengo la kuongeza ufanisi kiutendaji,” Mhe. Jenista ameongeza.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-UTUMISHI, Dkt. Laurean Ndumbaro akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kufungua kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, ofisi yake inatarajia kufanya tathmni ili kupima utekelezaji wa malengo yaliyowekwa katika kikao kazi cha mwaka jana na kuweka malengo mapya yatakayotekelezwa katika mwaka wa fedha ujao kwenye eneo la utumishi wa umma.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe akitoa salamu za Ofisi yake wakati wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
Sehemu ya washiriki wa kikao kazi cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akifungua kikao kazi cha siku mbili cha watumishi hao.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama akitoa zawadi ya shukrani kwa mwakilishi wa PSSSF ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa shirika hilo katika kuwezesha kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Mhe. Jenista ameongeza kuwa, Mhe. Rais amefanya kazi kubwa ya kusimamia na kutoa haki na stahiki kwa watumishi wa umma, hivyo ofisi yangu inao wajibu wa kukutana na wasimamizi hao wa rasilimaliwatu ili kuweka mkakati endelevu wa kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma.

“Tumeshuhudia Mhe. Rais amefanya mambo mengi mazuri kwa Watumishi wa Umma ikiwemo upandishaji wa madaraja, ulipaji wa malimbikizo ya mishahara, kutoa ajira na kupandisha mishahara kwa asilimia 23.3 kwa kima cha chini, hivyo watumishi tumuunge mkono kwa kufanya kazi kwa bidii bila kushurutishwa, weledi, uzalendo kwa taifa na kutoa huduma bora kwa wananchi,” Mhe. Jenista amesisitiza.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Alex Mfungo akitoa neno la shukrani kwa niaba ya washiriki wengine baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama kufungua kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala wa Utumishi wa Umma, Bi. Felister Shuli akiwasilisha mada kwenye kikao kazi cha siku mbili cha Wakuu wa Idara na Vitengo vya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma.

Kikao kazi hicho kinaongozwa na kaulimbiu isemayo “Utumishi wa Umma wenye Uadilifu, Nidhamu, Ubunifu, Weledi na Uwajibikaji wa Hiari kwa Ustawi wa Taifa”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news